JINSI YA KUANDAA NA KUANDIKA WIMBO WA KUSIFU AU KUABUDU.



HOW TO SING BETTER?
CLASSROOM
NA MWL, EV. MHUGO HANTISH (The sound of worship)
Tel number +255768788303


Mada: Jinsi ya kuandaa wimbo.
Nafahamu kwamba wengi waimbaji kama sio wote tuna mbinu mbalimbali za kuandaa, kuandika nyimbo. Wapo wanaoandaliwa na Roho mtakatifu kwa njia ya maono na ndoto, wapo ambao wenyewe hutumia mapigo Fulani ya ngoma au muziki uliandaliwa, wapo ambao wengine hukaa sehemu tulivu na salama kwa muda kidogo. Nk.

Sasa mie leo nakuletea mada hii jinsi ya kuandaa wimbo wako kiufasaha kabisa.

TAZAMA HAPA CHINI…






1. Pata wazo la kiujumla, la mada unayotaka au ujumbe unaotaka uuimbe. Kisha uhifadhi katika maarifa ambapo itakusaidia kujipambanua zaidi. Njia hii inakupa wepesi wa kuielewa mada au ujumbe wa wimbo unaotaka kuuandika.

2. Uandike ujumbe au mada yako kwenye kumbukumbu kisha
upende ujumbe wako au mada yako unayoiandaa ili ikupe fursa ya kuijadili zaidi. Kumbuka ya kwamba wewe ni kioo cha jamii, wewe ni mhubiri, wewe ni barua inayotakiwa kusomeka kwa watu wasioamini ili wapate kuamini. Hivyo unatakiwa kuielewa vyema mada au ujumbe unaotaka kusema au kuuhubiri. 

3. Baada ya kuuelewa ujumbe kisha uandike kwa ufasaha na kwa umakini kabla ya uimbaji au melody yake kuandaliwa.
4. Tathimini na ulinganishe ujumbe wa wimbo uliopo na wimbo uliouandika mwenyewe kabla hujautungia melody na kuuimba. Kuna waimbaji ukisikiliza wimbo wake alivyoimba labda kaimba mambo ya UPENDO WA YESU lakini alivyouita, kaita jina la  MIUJIZA YA YESU.









5. Soma sana na pitia sana Biblia kwa msaada wa Roho mtakatifu ili aweze kukusaidia kupata link  zinayofanana kwenye ujumbe wako.
Ikiwa inawezekana kufanya hivyo itafaa zaidi.

6. Huwa inaapendeza sana zaidi pale ambapo unaweza  kuzipangilizia verses zako au kama ni kwa mtindo wa mashairi ili kuepuka kurudia rudia maneno kama mtu aliye ishiwa maneno (mistari kwa lugha ya kawaida). s
7. Si utakua umeshaumaliza sasa kuuandikia wimbo kwenye ujumbe ule?. Hakikisha sasa kwa hatua ya mwisho halafu tayari kwa kuuimba acapella kwanza (inashauriwa kuimba bila beat ili ujipime kwanza mwenyewe kabla ya kuhitaji kusaidiwa na vyombo vya muziki.)








8. Utakua umeshakamilisha wimbo wako na tayari kwa kuurecord kwa maana ya kuuhifadhi katika compact disk (cd)kwa kuzingatia hatua au njia au mbinu hizo ninaamini Wimbo wako utapiga hatua kubwa kwa muda mfupi ndani na nje ya Roho za wasikilizaji na watazamaji wako wa ndani ya nchi hadi nje ya nchi. h


Powered By :                     

 

 "The voice to the voiceless"

 

       "The sound of worship"

TANGAZO

JE, UNAHITAJI KUTANGAZA HABARI YAKO HAPA www.hantishmhugo.blogspot.pe?

KAMA NI "NDIO" TUTUMIE EMAIL YAKO KWENDA hantishmhugo@gmail.comhantishmhugo@gmail.com AU gheadlinesleo@fmail.com UJUMBE/PIGA/WHATSAPP0768788303.

gospelheadlines@2018

"The voice to the voiceless"

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

SOMO:KUSIFU NA KUABUDU KATIKA BIBLIA.

HISTORIA YA MITUME WA YESU KRISTO NA VIFO VIFO

SOMO: MAONO NA NDOTO