GHL On Pre Sunday: MAJIBU YA PADRE KWA MUUMINI WAKE.

Tokeo la picha la padre with  womanMwanamke mmoja alimwendea Padre na kumwambia..."Sitaendelea kuja Kanisani..."

Padre akamuuliza, unaweza kuniambia kwa nini unasema hivyo?

Yule mwanamke akasema, "wakati wa ibada naona watu wakiwa wanatumia simu zao, wengine wakisengenya, wengine nao hawaishi ipasavyo kama Wakristo. Wote ni wanafiki tu."

Padre akakaa kimya. Kisha akamjibu yule mama, Sawa...Lakini nikuombe unifanyie jambo moja kabla hujafanya maamuzi?

Mwanamke akaitikia, "jambo gani hilo?"
Padre akamwambia, "chukua glasi ya maji na ulizunguke Kanisa mara mbili ukiwa nayo mkononi, na uhakikishe kwamba hakuna hata tone la maji linalodondoka."

Mwanamke akasema...."hilo naliweza kabisa!"
Akazunguka Kanisa mara mbili akiwa na ile glasi ya maji na akamrudia Padre na kumwambia kwamba, "nimekamilisha."

Baada ya kuona vile, Padre akamuuliza maswali matatu:

1. Uliona mtu yeyote akiwa anatumia simu yake?
2. Uliona mtu yeyote akiwa anasengenya?
3. Je, uliweza kumwona mtu yeyote aliyekuwa anaishi visivyo?

Mwanamke akajibu kwamba, "Sikuona chochote kwa sababu nilikuwa makini nikiitazama hii glasi ili maji yasimwagike."

Padre akamwambia, "Unapokuja Kanisani, unapaswa kuwa makini na kwakumwelekea Mungu tu ili usianguke. Ndiyo maana Yesu alisema, "NIFUATENI!!" Hakusema tuwafuate Wakristo. Hivyo, usikubali mahusiano yako na Mungu yaongozwe na jinsi watu wengine wanavyohusiana naye. MAHUSIANO YAKO NA MUNGU YANAPASWA KUONGOZWA NA NAMNA AMBAVYO WEWE MWENYEWE UNAHUSIANA NAYE."


Tuachie maoni yako hapo chini.

JE, UNAHITAJI KUTANGAZA HABARI YAKO HAPA www.hantishmhugo.blogspot.pe?

KAMA NI "NDIO" TUTUMIE EMAIL YAKO KWENDA  hantishmhugo@gmail.com AU gheadlinesleo@fmail.com UJUMBE/PIGA/WHATSAPP0768788303.

=TUNAPATIKANA PIA YOUTUBE CHANNEL, FACEBOOK PAGE NA INSTAGRAM ACCOUNT.

gospelheadlines@2019

"The voice to the voiceless"

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

SOMO:KUSIFU NA KUABUDU KATIKA BIBLIA.

HISTORIA YA MITUME WA YESU KRISTO NA VIFO VIFO

SOMO: MAONO NA NDOTO