Ruka hadi kwenye maudhui makuu

TULIOMBEE BUNGE LA TANZANIA.

facebook

Ev. Mhugo Hantish the sound of worship.
Habari mpenzi mwanamedia! Natumaini uheri wa afya njema ikiwa umepata fursa ya kusoma ukurasa huu.       Leo ni mara yangu ya kwanza kuandika makala hii inayohusiana na masuala ya kisiasa nchini. Lengo thabiti ni kutamani na kushawishi sote waumini wa dini na madhehebu (yote)mbalimbali yanayomcha Mungu kwa pamoja na umoja wetu popote pale tulipo kumkabidhi Mungu jambo hili (bunge, wabunge pamoja na shughuli za kibunge.) Ifahamike kuwa bunge kazi yake ni kuisaidia na kuishauri lakini pia kuikosoa serikali. Sanjali na hilo wabunge ndio wahusika wakuu wa kuikosoa serikali hiyo.. (Na hii ni nchi nyingi afrika na dunia kwa ujumla wanafanya hivyo). Sitamani kusema ni mpinzani wa UKAWA bali nataka kuweka mtazamo chanya na kuifanya nchi hii iwe na amani siku zote. Leo imekua kawaida sana kusikia ama kushuhudia wabunge wa upinzani wakipinga baadhi ya mambo au mipango iliyowekwa mezani mbele ya spika wa bunge. Hali hii imezidi hadi kufikia kutomtaka naibu spika aliyepo na kufikia hatua ya kudiriki kutengeneza hoja za kumuondoa kitini. Haijaishia hapo... Bado imefikia chuki imetanda hadi mbunge kwa mbunge wananuniana.
      Tukumbuke jambo moja kuwa mbungeyeyote yule akiwa bungeni ni mwakilishi wa wananchi wake jimboni. Dhana hiyo sasa inaanza kama kusahaulika hivi na kujiingizia maslahi binafsi. Yaani hata profesa daktari anaacha kuitumia taaluma yake kwa maendeleo ya taifa lake anagambania ubunge kwa maslahi yake binafsi.
Sasa basi leo niwaombe watanzania wenzangu wote kwa dini zetu na madhehebu yetu tumwinamie Mungu aturehemu na pia aturejeshee umoja ndani ya bunge ili mijadala ijadiliwe kwa amani na utulivu. Kwa kufanya hivyo sie tutakua chachu ya mabadiliko pale bungeni kwa sababu Mungu atakwenda kushuka moja kwa moja ndani ya mioyo wa wabunge wote bila kujali itikadi zao. Usisahau kumwombea mbunge wa jimbo lako utokako.
    "Bwana nenda nasi" " hatutoki hapa kama usipo enda nasi"
Huenda kuna wakati wabunge wameenda peke yao ndio màna mipango mingi au baadhi imegonga ukuta.. "Ninyi ni nuru ya ulimwengu, mji hauwezi kusitirika pasipo ninyi"
           MUNGU atutangulie...!
!  
         Na ubarikiwe kwa kufanya hivyo!!
 — feeling thoughtful at Bungeni Dodoma.
Yesterday at 3:43pm · Public · in Timeline Photos
View Full Size · Edit Photo · Send as Message
2 people like this.

Benson Lupila

Amen
Like · Reply · Message · Delete · Report · Yesterday at 8:25pm

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

SOMO:KUSIFU NA KUABUDU KATIKA BIBLIA.

HISTORIA YA MITUME WA YESU KRISTO NA VIFO VIFO

SOMO: MAONO NA NDOTO