Judith Mbilinyi - Maisha Yangu Official Video
Bwana Yesu Asifiwe! Mpendwa msomaji wa blog yetu pendwa ya GOSPEL HEADLINES LEO, leo kwa uwezo wa Mungu nimekusogezea video ya wimbo wenye baraka nyingi sana uitwao Maisha Yangu kutoka kwa mwimbaji mahiri wa nyimbo za injili kutoka jijini Dar es salaam Tanzania anayefahamika kwa jina la Judith Mbilinyi. Wimbo huu wa kuabudu umetayaarishwa katika studio za EM Records chini ya mikono thabiti ya mtayarishaji Erasto Augustino. Hii ni moja kati ya nyimbo zenye mafuta ya pekee sana ya upako katika kumwabudu Mungu ambaye kupitia Bwana wetu Yesu Kristo ameachilia nguvu ya ajabu kwa mtumishi Judith Mbilinyi ambaye kupitia wimbo huu ameonekana kuwa katika uwepo wa kipekee wa Mungu akilisifu jina la Yesu Kristo na kuzikumbusha nafsi zetu pia kuwa maisha yetu yapo mikononi mwa Bwana wetu Yesu. Ili kuutazama wimbo huu ambao upo kwa mfumo wa video, bofya hapo chini. Karibu sana. Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na Judith Mbilinyi kupitia: Simu ...