WAIMBAJI: TUNDUMA KUMEKUCHA KWA YESU
WAIMBAJI: TUNDUMA KUMEKUCHA KWA YESU.
Na Mwandishi wetu,
SONGWE,
Umoja wa waimbaji wa nyimbo za injili mkoa wa Mbeya na Songwe, kwa pamoja umeendelea kushika hatamu kwa kile kinachoelezwa kuwa NGUVU YA USHIRIKIANO imeishibisha huduma ya uimbaji iliyomo ndani ya vipawa vya waimbaji hao. Umoja huo ambao hadi sasa unakadiriwa kuwa na jumla ya waimbaji takribani 200, ambao licha ya kuwa na huduma ya mmoja mmoja lakini umeendelea kushirikiana katika kuifanya huduma hii ikiwa ni pamoja na kuandaa mikutano, mikesha na makongamano yenye lengo la kujifunza neno la Mungu pamoja na wakristo wengine mahali popote.
Kwa kulitambua dhumuni la Umoja huo na kwa kutambua jukumu la kila mwimbaji anayehusisha umoja huo na kwa kutambua umuhimu wa kumtumikia Kristo aliye tumaini letu, viongozi wa kamati kuu tendaji ya Mkoa wa Mbeya kwa niaba ya waimbaji, wameratibu maandalizi ya Kongamano kubwa la neno la Mungu litakalo fanyika Mkoa wa Songwe-Tunduma mnamo tarehe 16 hadi 18 Machi 2018 (siku 3). Mahali ni P.H.A.M.T - NGUVU YA UKOMBOZI, KALOLENI IDARA YA MAJI. Kongano hilo linatarajiwa kuhudhuriwa na (watumishi) wachungaji na waimbaji mbali mbali wakiwemo:- Tumain Mbembela, Iman John, Yakobo Mwamboya, Ikupa Mwambenja, Neema
Jackson, The Twins Dadaz, Pinty Melody, Mc Joshua Mwakabela, Emmanuel
Mwansasu, Happy Sanga, Ipyana Mwakatika, Afande Bright, Juma
Kyando/Kibonge wa Yesu, Patrick Mwaibambe, Ev Mhugo Hantish, Kefa
Malimali, Onesmo Nickodem, Emmanuel Mwakapughi, Kepha Kialo, Fidia Tinga, Angela Chisa, Angel Thomas, Daniel Samaria, Babycia Samaria, Ayubu Samaria, Rahabu Mwasibata na wengine wengi.
Hivyo kwa kutimiza kusudi la Mungu, unaalikwa ewe msomaji na yeyote utakaye pata taarifa hizi leo ya kwamba hupaswi kulikosa kongamano hili kwani hakutakuwa na kiingilio, ni bure kabisa. Andaa moyo wako kwaajili ya kupokea.
PICHA KWA HISANI YA HINJU ZE ONE, DH
Wanaohitaji afya na kuombewa haja zao watapatiwa huduma hizo kutoka kwa watumishi wapakwa mafuta na Bwana.
NYOTE MNAKARIBISHWAAAA...!!!
Maoni
Chapisha Maoni