KILIO CHA YATIMA
Nickson Mahundi - Kilio cha Yatima (Official Video)
KILIO CHA YATIMA
Haleluya mpendwa msomaji wa blog yetu pendwa ya GOSPEL HEADLINES LEO . Leo nimekusogezea wimbo uitwao KILIO CHA YATIMA. Wimbo huu ulioimbwa na mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka nchini Tanzania, NICKSON MAHUNDI umebeba kusudi la kuwatetea watoto yatima na wote waishio katika mazingira hatarishi, ambao wamekosa malezi na huduma mbalimbali za kiafya na kijamii. Mwimbaji huyu ambaye pia ni mwanahabari na mtangazaji mahiri, amefanyika faraja sana katika maisha ya watoto yatima na hasa waishio maisha ya mtaani.
Licha ya huduma yake ya uimbaji na utangazaji lakini
pia NICKSON MAHUNDI ni 'Managing director' wa kituo cha utangazaji cha
Redio Best Fm 90.3 mHZ kilichopo Mkoani Njombe, Wilaya ya Ludewa.
Nikukaribishe
kuitazama video hii kwa moyo mmoja, naamini utajifunza kitu kupitia
ujumbe huu wenye harufu ya UDIAKONIA ndani yake.
<BOFYA NA TAZAMA HAPA VIDEO HIYO
<BOFYA NA TAZAMA HAPA VIDEO HIYO
Maoni
Chapisha Maoni