Ruka hadi kwenye maudhui makuu

SOMO: MWALIKO WA YESU NYUMBANI KWA MARTHA NA MARIAM. Luka mt. 10:38-42

facebook

Ev. Mhugo Hantish the sound of worship.
Ikawa katika kuenda kwao aliingia katika kijiji kimoja mwanamke mmoja aitwae Martha alimkaribisha Yesu nyumbani kwake.huko Martha alikua na mdogo wake aitwae Mariam, aliyeketi chini pa Yesu akisikiliza maneno take.
Lakini Martha alikua akijishughulish
a kumwandalia chakula Yesu. Alipoona yu peke akamwendea Yesu na kumwambia "Bwana huoni vibaya hivyo ndugu yangu alivyoniachia kazi peke yangu? Basi mwambie anisaidie." Bwana akajibu "Martha Martha unahangaika na mambo mengi lakini linatakiwa jambo moja tu. Na Mariam amechagua fungu lililo jema ambalo hataondolewa." Luke 10:38-42
Bwana Yesu Asifiwe!!!!! Kimsingi kuna wanawake wengi katika biblia ambao wametenda mengi ya kujifunza sie kimwili na kiroho pia.
Vifungu hivyo vinne vya Biblia vinatuongoza kujifunza namna ya kuishi maisha ya kiroho pasipo kuathiri maisha ya kimwili.
Wakati Mariam akimsikiliza Yesu Martha alikua akihangaika huku na kule ili kutengeza chakula cha yesu pamoja na wafuasi wake. Hii ni desturi yetu kimwili katika kukarimu wageni.
Hebu mpendwa mwenzangu tujiulize kwa nafasi zetu wenyewe nani aliye na kosa hapo? Kwasababu Mariam alitambua ugeni ule ni ukombozi kwake lakini martha alitambua kuwa ugeni ule una hitaji kuondolewa uchovu angalau kwa chakula kidogo. 

MAMBO YA KUJIFUNZA KIMWILI

Martha alikua mkarimu kwa wageni.
Aliwapenda, alionyesha upendo dhidi ya wageni. 

JAMBO LA KUJIFUNZA KIROHO.
Alimweleza Yesu shida aliyokutana nayo. Hakumlalamikia ndugu yake moja kwa moja. Hivyo nasi tujifunze kumweleza Yesu shida zetu.

Hitimisho.: 
Yesu alifananishwa km ni mtatuzi na msuluhishi WA matatizo ya kimwili na kiroho. Yesu wa enzi zile za martha na Mariam hata leo ndiye huyo. Kama bado unaishi amini kuwa amekutembelea Yesu maishani mwako. Kipi umejifunza kwa Yesu?
Pia kwa kumalizia tu: tujifunze kubalance majukumu. Muda wa kushiriki kiroho utumie vema pasipo kuathiri muda wa majukumu ya kimwili. Na muda WA majukumu ya kimwili husika kikamilifu pasipo kuathiri muda wa kiroho. Katika hili utakuta mtu anashinda kansani au nyumbani kwa mchungaji kutwa nzima, siku nyingi katika juma hadi anasahau majukumu ya nyumbani. Kama ni mwanamke wa ndoa unaweza sababisha ikawa ndoano ...

Mungu akusaidie sana. Barikiwa

4 hours ago near Masasi · Public · in Timeline Photos
View Full Size · Edit Photo · Send as Message


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

SOMO:KUSIFU NA KUABUDU KATIKA BIBLIA.

HISTORIA YA MITUME WA YESU KRISTO NA VIFO VIFO

SOMO: MAONO NA NDOTO