WITO WANGU KWA MANABII, WACHUNGAJI NA WAIMBAJI
Ev. Mhugo Hantish the sound of worship.
Wito
kwa manabii wote wanaotumia neno la Mungu. Tumieni neno la Mungu
kuwaokoa wanadamu na kuwaponya Miili yao na Roho zao. Wengi wamekua
wakiwaponya wagonjwa wa kimwili na wanasahau wagonjwa wa Mioyo. Lakini
Pia msiiuze injili ya Mungu iliyoletwa na Yesu mwanae. Tunahubiri kwa
sababu kuna watu wana dhambi lakini hatupaswi kuhubiri kwa sababu watu
wana fedha na mali kwaajili yetu.. La hasha. Hivyo tuitangaze injili ya
Yesu ambayo ilikuwa na lengo la kuja kukitafuta kile kilichopotea.
Wachungaji wengi tumeegemea kwenye kuihubiri injili kibiashara. Hapa
nieleweke vizuri. Kuna watumishi wengine hasa waimbaji wa nyimbo za
injili wakiitwa kuhudumu mahali fulani utaskia "niandalie milioni moja"
MTU WA Mungu uliyekomaa sidhani kama unaweza fikia hatua hiyo. Ukiinuliwa usijiinue, umepewa nafasi ya kubinya unataka kutoboa inawezekanaje.. ?
Muhubirini Mungu, acheni kujitukuza wenyewe na kumsahau muumba WA mbingu na nchi. Wapo manabii wanaotumia madhabahu yao kujitutumua na hata makanisa yamepewa majina yao wenyewe. Hofu yangu ni kwamba tusije fikia hatua tukasau kumtangaza kristo aliyetufanya tuwe hapa tulipo.
Kama sote tunamtangaza Kristo kwa kutumia Biblia moja basi tuwe wamoja. Kadri siku zetu zinavyosogea wachungaji WA makanisa tofauti wamekuwa wagomvi "indirect" hali iliyopelekewa waumini nao kuona ni tofauti na wa dhehebu lingine. Mungu aturejeshee upendo na amani inayotaka kupotea.
Neno la Bwana likanijia kusema "mwanadamu uiambie wewe u nchi isiyo safika wala kunyeshewa mvua siku ya ghadhabu. Fitina ya manabii wake ipo ndani yake kama simba aungurumaye akirarua mawindo......" Ezekieli 22:23-25 Mungu awalinde na kuwabariki.
MTU WA Mungu uliyekomaa sidhani kama unaweza fikia hatua hiyo. Ukiinuliwa usijiinue, umepewa nafasi ya kubinya unataka kutoboa inawezekanaje..
Muhubirini Mungu, acheni kujitukuza wenyewe na kumsahau muumba WA mbingu na nchi. Wapo manabii wanaotumia madhabahu yao kujitutumua na hata makanisa yamepewa majina yao wenyewe. Hofu yangu ni kwamba tusije fikia hatua tukasau kumtangaza kristo aliyetufanya tuwe hapa tulipo.
Kama sote tunamtangaza Kristo kwa kutumia Biblia moja basi tuwe wamoja. Kadri siku zetu zinavyosogea wachungaji WA makanisa tofauti wamekuwa wagomvi "indirect" hali iliyopelekewa waumini nao kuona ni tofauti na wa dhehebu lingine. Mungu aturejeshee upendo na amani inayotaka kupotea.
Neno la Bwana likanijia kusema "mwanadamu uiambie wewe u nchi isiyo safika wala kunyeshewa mvua siku ya ghadhabu. Fitina ya manabii wake ipo ndani yake kama simba aungurumaye akirarua mawindo......" Ezekieli 22:23-25 Mungu awalinde na kuwabariki.
— supporting Positive thinking at .
Today at 10:13am · Public · in Timeline Photos
View Full Size · Edit Photo · Send as Message
Maoni
Chapisha Maoni