ALICHOSHAURI MCHUNGAJI ABIUD MISHOLI.
"Hiyo
picha nikiwa Moshi bomang'ombe nikiendelea kuhubiri habari ya ubaya wa
Dhabi. Ngoja nikupe sababu ya pili kwanini usitende dhambi tena.
Usitende dhambi tena kwasababu dhambi moja inaongeza dhambi nyingine.
Mimi nimeshawahi kuvuta bangi japo si sana kama wewe. Usiumie kwa hilo
neno kama hauvuti. Ila chanzo cha kuvuta kwangu kwanza kilitokana na
marafiki wabaya hao ndio kwanza walionifundisha sigara, haikuishia hapo
ndio wakanifundisha bangi, haikuishia hapo wakaanza kunipeleka
disco. Kwa Hiyo kila siku nikawa naongezeka katika uovu. Na ndomana
kama kuna kitu nawaombea watoto wangu sana. Ni hichi Mungu awaepushe na
marafiki wabaya, chuma hunoa chuma, mtu mwenye nguvu huinua mwenye
nguvu. Huwezi ukatembea na mtu mwenye neema na uwezo, kama akili zako
zimetulia na mpenda maendelea usiendelee, lazima ubadilike. Na kumbuka
rafiki anasehemu kubwa kwenye maisha ya mtu. Na ndomana wakati flani
Mungu alipotaka kufanya jambo kubwa na mtu alimtenga. Hata wewe japo si
wote unayesoma kipande hichi. Kuna mambo ambayo umeingiziwa na watu,
umepozwa na watu. Umesabishiwa na watu. Na Hata dhambi umefundishwa na
watu. Nakupa shauri funga mlango, au mwanya wowote uliokuwa unaupuuza,
uliokuwa unakuingizia tabia moja mbaya. Leo jua kwamba Hiyo tabia moja
mbaya kesho itazaa mapacha na msururu wa tabia nyingi mbaya. Hata wewe
ni shaidi japo sio wote siku ulipoangalia picha ya ngono. Ikazaliwa
dhambi nyingine ya kujichua. Ukaona haitoshi ukatafuta na mtu wa kuzini
naye. Na sasa si mmoja umeshakuwa na wengi. Lakini mwanzo wa haya yote
ulifungulia tabia moja mbaya kwenye maisha yako. Na hiyo tabia moja ndio
imezaa hizo tabia nyingine .Nakushauri na Mungu ni shaidi usitende
dhambi tena. Ukoka kwakumaanisha, na Mungu akusaidie."
Maoni
Chapisha Maoni