PICHA 10+ ZA HARUSI YA HANTISH MHUGO NA FARIDA KILASI TAR 01.10.2016
Mr.Jozack(mzazi) Mhugo katika kusherehekea...
...Bi. Anna Haule amejawa na furaha....
..kwaya mbalimbali zilikuwepo katika tukio...
...ni katika kusaini vyeti vya ndoa..
Ev. Mhugo Hantish akitoa neno la shukrani baada ya kufunga ndoa dakika chache zilizopita.
....Farida Kilasi akisaini vyeti vya ndoa..
Mr. Jozack Mhugo akitoa wosiakwa mwanae Hantish katika ibada
ndugu wa Hantish Mhugo wakisikiliza jambo toka kwa mchg. Masawa(picha ya chini)
......wametoka ibadani ....
...maharusi wanapeleka keki kwa wazazi wao...
hakika walipendeza, ilikua ni siku ya aina yake ambapo wengi walijitokeza kushuhudia tukio maalum la Ev. Mhugo Hantish akifunga pingu za maisha na Farida Kilasi huko usuka, Wilaya ya Wanging'ombe, Mkoani Njombe Tanzania.
Maharusi wakilishana keki kwa style ya ajabu.
........style nyingine hiyo ya kulishana keki(picha na Hekima Mhugo)
keki iliyotengenezwa na kusafirishwa toka Dar-es-Salaam Ubungo, 5star (picha na Hekima Mhugo)
Hatimaye Bw. Hantish Mhugo mwimbaji wa nyimbo za injili auaga ukapela. ayaanza rasmi maisha ya ndoa.
ndoa yake iliyofungwa tar 01.10.2016 huko mkoani njombe iliwafanya wakazi wengi wa maeneo hayo kuhudhuria kulishuhudia tendo adimu kabisa.
"tunamshukuru sana Mungu kwa kutufikisha siku hii ya leo, hakika imekua ni furaha sana kwetu na ya baraka kwetu" alisema Hantish Mhugo muda mfupi mara tu baada ya kukamilisha jambo la harusi alipokua akiongea na moja ya gazeti linaloripoti habari za wasanii wa Muziki nchini Tanzania.
Hata hivyo amewashauri wanamuziki wengine wanaojihusisha na muziki kutimiza kusudi la Mungu maana ni njia tunayoipitia. "..hivi sasa nimekamilisha moja kati ya maagizo ya Mungu kama Biblia inavyoeleza.. nawashauri na wenzangu kutii maagizo ya Mungu maana hii ni njia ambayo kila mmoja ni haki yake kuipitia ikiwa yu hai na mwenye pumzi." aliongeza mwimbaji huyo anayemiliiki Bendi ya muziki wa injili inayoitwa "The winners band" inayofanya vizuri katika Muziki wa injili.
Maoni
Chapisha Maoni