Mhugo Hantish. Behind the scene. #ainuliwe Mungu wetu
hatimaye msanii wa nyimbo za injili HANTISH MHUGO maarufu kwa jina la Ev Mhugo Hantish the sound of worship aingia location kuitengeneza video ya wimbo wake mpya unaoitwa AINULIWE MUNGU WETU. AUDIO imetengenezwa na PRODUCER TINO katika studio za PLASTER MUSIC-SONGEA, VIDEO IMETENGENEZWA na HINJU ZE ONE katika studio za HINJU VIDEO AND FILM PRODUCTION COMPANY ikishirikiana na MSAMARIA VIDEO PRODUCTION.
Ilikua ni tar 23.11.2016 ndipo video ilipo shoot. na audio iliachiwa tar 1.11.2016.
Ev. Mhugo Hantish ambaye amekua kwenye huduma kwa takribani miaka saba sasa ameeleza furaha yake wakati akizungumza na chanzo cha habari na kwamba jitihada bado zinaelea kufanyika ili kuhakikisha tasnia ya mziki wa injili inafika mbali zaidi ya hapa ilipo sasa. aliongeza zaidi mzee wa NIKUPE NINI MWILI kwamba haoni sababu ya kuacha au kusimama kufanya huduma ya uinjilist kupitia nyimbo maana ni karama ya kutoka kwa MUNGU na hivyo aliwasihi waumini wa madhebu na dini zote kulitambua kusudi la MUNGU na kuliishi.
kila mwanadamu awaye yeyote anayo sababu ya kuisikiliza sauti ya Mungu ili apate kutambua ni nini kusudi la Mungu kumfanya aishi hadi leo hii
Maoni
Chapisha Maoni