DARASA LA UIMBAJI
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
VOCAL TRAINING - DARASA LA UIMBAJI
John Shabani akiwa na baadhi ya wanafunzi wenzake wa sauti
John Shabani akisimamia waimbaji katika kuandaa wimbo wa miaka 50 ya uhuru wa Tanzania
J- SINGING LESSONS (Mafunzo ya sauti na uimbaji)
SINGING COURSE
Darasa hili la sauti na uimbaji linaendelea, njoo darasani, utajifunza mengi zaidi.
Piga simu namba 0713778778 na 0754818767 ili upewe maelekezo ya tunapopatikana na muda wa darasa.
0716 560094
Haya ni masomo machache
sana niliyoyachagua kati ya mengi ili kukupa hamasa kujiunga na darasa la
uimbaji linaloendelea jirani na Landa mark Hotel Ubungo chini ya mwalimu John
Shabani na timu yake
Karibu ujifunze
Mambo ya msingi yanayofunzishwa katika program hii:
· Tofauti
ya mwimbaji na mwanamuziki
·
Vyakula
na vinywaji vinavyofaa na visivyofaa kwa mwimbaji
·
Sifa na
mbinu za kuwa mwimbaji bora
·
Jinsi ya
kuitunza na kuiponya sauti yako
·
Amri 10
za sauti/uimbaji
·
Matumizi
ya kipaza sauti (Microphone technique)
·
Utunzi wa
nyimbo
·
Sifa 4 za
kuwa na Album bora
·
Nguzo 4
za muziki
· Funguo (Keys) 7 za
muziki
·
Mazoezi
ya viungo yanayofaa kwa mwimbaji na faida zake
·
Ushauri
kwa wanaotaka kurekodi nyimbo
Kuimba ni kutamka maneno katika hali ya ki-muziki au pia
twaweza kusema ni kutamka maneno moja baada ya jingine kwa sauti yenye lahani
(sauti ya ala ya muziki, tuni) au ghani (Singing is the act of producing musical
sounds with the voice)
Mwimbaji ni mtu yeyote mwenye uwezo wa kuimba au
bila vyombo vya muziki (be sung a cappella) au kwa kutumia
vyombo. Mwimbaji huyo kwa lugha ya ki-muziki anaitwa vocalist. Ikumbukwe kuwa
pia katika vikundi vya uimbaji wapo wale wanaoongoza wengine katika uimbaji (A lead
singer) na wengine kazi yao ni kuitikia (backing singers)
N.B
Mwanadamu yeyote
mwenye uwezo wa kuongea, anauwezo wa kuimba pia.
Kama vile tulivyo na ala za aina mbalimbali, mwimbaji naye pia anazo ala
mbili muhimu:
Mdomo
wenye uwezo wa kutoa sauti ya uimbaji
Mwili
Kumbuka moja ya
vitu vya msingi katika uimbaji ni nguvu (energy)
Mckinney alisema: “As
you sing higher, you must need more energy, as you sing lower, you must
useless; as you sing higher, you must
use more space; asa you sing lower, youmust need use less””. Inamaanisha
kadri unavyotumia sana sauti hasa kwa sauti ya juu sana, ndipo unapohitaji pia
nguvu kubwa, japo wapo watu kwasababu ya uzoefu wa kuimba kwa muda mrefu au
kupitia madarasa kama yale yanayofundishwa na mwalimu John Shabani, kwo kuimba
sauti ya juu au ya chini ni jambo la kawaida.
Zipo nguvu za kiroho na za kimwili. Ili kuwa
na nguvu za kimwili unahitaji maji ya kutosha, chakula kizuri, hewa pamoja
na mazoezi ya viungo maalum kwaajili ya uimbaji au ya pumzi.
Mwimbaji pia
anahitaji Pumzi ya kutosha (Breathing support), chakula kizuri na maji ya
kutosha
Funguo (Keys) 7 za muziki
C-do, D-re, E-mi, F-fa, G-sol, A-la, B-si
Lakini kwenye skeli (scale) ziko funguo (keys)
8 : do re mi fa sol la ti do, na kila funguo ina ngazi 8. Hivyo kwa mafunzo ya
sauti kila key inawezakuwa do. Chamsingi usiimbe flat, sauti yako iwe na nguvu
(strong on key), isiwe dhaifu (weak).
Tunaipata key kwa njia mbili: wewe mwenyewe
kujitafutia au kusaidiwa na chombo cha muziki. Wewe mwenyewe ukijipa key,
waweza kubadili, lakini ukipewa key na chombo huwezi kwenda kinyume.
Hakuna wimbo unaweza kuimbwa katika funguo
zote saba, bali ufunguo (key) 1 moja ye mabadiliko ya ngazi kadhaa kati ya hizo
8. Ninaposhuka key ninaita hiyo ni flat na nikipanda chumba hiyo ni sharp,
lakini key E na B hazina sharp. Tofauti ya key moja kwenda key nyingine ni
vyumba viwili unapokuwa unatumia vyomvo vya muziki.
Kuimba kwenye tempo ni kuimba kwa kufuata mapigo ya drum au aina yoyote
ya ngoma au mshindo
Ikiwa mwimbaji hajajua kuimbia
kwenye funguo (key) na mapigo au mdundo
(beat) bado huyo anatatizo kubwa. Hakuna muziki wa zamani na wa sasa, isipokuwa
nyimbo ndio zinaweza kuwa za zamani.
MAADHI YA MUZIKI DUNIANI
Tunaposema maadhi tuna maanisha mtindo fulani wa muziki au uimbaji.
Kuna maadhi ya aina nyingi duniani, yapo maadhi ya Nchi, maadhi ya
Kabila maadhi ya Dini, maadhi ya koo n.k
Ili unielewe vizuri hapo chini ni maadhi kadhaa:
Rumba, Reggae, chakacha, kwela, kwaito, Sukous, sebene, rock, pop n.k
Sauti ni mlio wa chochote kinachoweza kusikika
SIFA ZAKUWA MWIMBAJI BORA
Sauti, kwenda na mapigo na kusimama kwenye ufunguo (Key),
mwonekano, (appearance), Uwezo wa
kuitumia sauti na kuitawala (Manage your vocal), Stage presence (Muonekano
jukwaani), kujiamini, kujitambua, kujithamini Self Cofidance), kuwa na sikio la
muziki, kuwa mbunifu na kujitengenezea swaga zako binafsi huku zinazoendana na
muonekano wako usoni na mwili mzima. n.k.
HATUA 4 ZA KUREKODI AU KUWA NA ALBAM BORA
1.
Mwimbaji kuwa bora
2.
Tungo au ujumbe bora
3.
Muziki bora
4.
Studio bora
NGUZO
4 ZA MUZIKI
1.
Kusikiliza muziki/uimbaji (Listening)
2.
Kuhifadhi muziki/uimbaji (Copying)
3.
Kuiga au kukariri (meditate)
4.
Kuzalisha muziki (producing)
Mazoezi kwa mwimbaji
Yapo
mazoezi maalum kwaajili ya kuboresha uimbaji na pia kumfanya mwimbaji awe na
ngu ya kutosha na kuepukana na baadhi ya magonjwa. Kwa ushauri zaidi wasiliana
na mwalimu John Shabani.
Pamoja na faida
nyingi za mazoezi lakini pia mazoezi huchangamsha mwili, hulainisha koo,
husaidia kuwa na pumzi ya kutosha, hukuhepusha au kupunguza baadhi ya magonjwa
kama kisukari, presha n.k, hung’arisha ngozi, na kusaidia mfumo wa mzunguko wa
damu, mazoezi husaidia katika mfumo wa usagaji chakula kuwa mzuri , kukupa
nguvu na kuweza kufanya kazi kwa nguvu zako bila kujiskia umechoka na mwisho wa
siku hupunguza mafuta mwilini, hupunguza
uzito, kunyoosha na kuimarisha misuli ya mwili, husaidia mapigo mazuri ya moyo
kwa kuongeza kasi ya mapigo yake wakati wa mazoezi, unguza mrundiko wa damu
kwenye mishipa, hii ni muhimu kwa sababu mgando wa damu husababisha magonjwa ya
moyo pamoja na kupoteza fahamu, mazoezi huimarisha mifupa ya mwili, huboresha
usingizi ambao unafaida sana kwa mwimbaji.
Tafadhali, inawezekana lugha niliyoitumia hujaielewa sana, nawakati mwingine
nimechanganya na kingereza au lugha ya muziki. Ikumbukwe kuwa muziki una lugha
yake, na pia nimejaribu kutafsi kutoka kwenye notisi zangu ambazo mimi mwenyewe
najifunza kwa lugha ya kingereza. Lakini kwa ushauri zaidi tuwasiliane.
Kumbuka muziki au uimbaji ni kama bahari, kila mtu anaogelea pale
anaweza kufiki, mimi naweza nikakutoa hapa nikakupeleka pale, na mwingine
akakutoa pale na kukupeleka kwingine. Hakuna aliyefika kikomo cha kujua muziki
au uimbaji, sote ni wanafunzi, na pia katika kufundishana sote tunajifunza.
Ikiwa unataka kuwa mwimbaji bora, na unahisi bado unatatizo fulani
tuwasiliane.
Jinsi ya kuponya na kutunza Sauti yako
By
John Shabani
Weka
sauti yako katika afya nzuri ili uweze kuendelea kuimba!
Kila mtu anaweza kutumia sauti yake, lakini
si kila mtu anajua jinsi ya kutunza afya ya sauti yake, au nini cha kufanya kunapotokea tatizo katika sauti. Makala hii itasaidia kila mtu kujifunza jinsi ya kuponya
sauti zao na pia kutoa ushauri wa jinsi ya kutunza afya yake na kuwa nguvu ile ile
kwa ajili ya siku zijazo.
Mambo unayo hitaji au ya kuzingatia kama mwimbaji
- Fanya mazoezi ya pumzi kadiri uwezavyo
- Kunywa maji ya moto kadiri uwezavyo
- Epuka kupaza sauti au kupayukapayuka bila mpangilio
- Pia mvuke wa maji yaliochemsha husaidia
Maelekezo
o
1 Kama sauti yako imejeruhiwa, jambo muhimu zaidi la kufanya hivi sasa ni
kuacha kutumia kwa muda. Sauti inahitaji kupumzika pia. Punguza mazungumzo yako na hasa kupayuka na kupaza sauti,
kujifunza kuzungumza zaidi kwa ufupi, na kutumia zaidi kidogo muda katika
ukimya.
o 2 Jambo jingine kubwa
ambalo husaidia sauti iliojeruhiwa ni chai ya moto pamoja na limau kidogo na asali. chai nzuri ni ile iliyo shauriwa ki afya na si kila chai ni bora. Unaweza kupata na dawa za mitishamba katika duka
la dawa, ambazo ni maalumu kwa ajili ya
sauti, Kunywa angalau kikombe asubuhi na kikombe wakati wa usiku.
o 3 Nini kama kulikuwa
na kitu ambacho kingeweza kusaidia kuponya sauti yako na pia kutumika kulinda
kila siku? Ni wito wangu kwako Kunywa kwa wingi kila siku. maji
husaidia sauti kuwa hidrati. Kukaa hidrati husaidia kuweka mwili wako na afya
na sauti yako tayari kufanya kazi!
John Shabani akiongoza sifa
Moja ya huduma za John Shabani
Marehemu Debora shabani akihudumu
Mwalimu John akiongoza mazoezi yapumzi
Joyce John akijifunza kupiga kinanda
Darasa hili la sauti na uimbaji linaendelea, njoo darasani, utajifunza mengi zaidi.
Piga simu namba 0713778778 na 0754818767 ili upewe maelekezo ya tunapopatikana na muda wa darasa.
0716 560094
Haya ni masomo machache
sana niliyoyachagua kati ya mengi ili kukupa hamasa kujiunga na darasa la
uimbaji linaloendelea jirani na Landa mark Hotel Ubungo chini ya mwalimu John
Shabani na timu yake
Karibu ujifunze
Mambo ya msingi yanayofunzishwa katika program hii:
· Tofauti
ya mwimbaji na mwanamuziki
·
Vyakula
na vinywaji vinavyofaa na visivyofaa kwa mwimbaji
·
Sifa na
mbinu za kuwa mwimbaji bora
·
Jinsi ya
kuitunza na kuiponya sauti yako
·
Amri 10
za sauti/uimbaji
·
Matumizi
ya kipaza sauti (Microphone technique)
·
Utunzi wa
nyimbo
·
Sifa 4 za
kuwa na Album bora
·
Nguzo 4
za muziki
· Funguo (Keys) 7 za
muziki
·
Mazoezi
ya viungo yanayofaa kwa mwimbaji na faida zake
·
Ushauri
kwa wanaotaka kurekodi nyimbo
Kuimba ni kutamka maneno katika hali ya ki-muziki au pia
twaweza kusema ni kutamka maneno moja baada ya jingine kwa sauti yenye lahani
(sauti ya ala ya muziki, tuni) au ghani (Singing is the act of producing musical
sounds with the voice)
Mwimbaji ni mtu yeyote mwenye uwezo wa kuimba au
bila vyombo vya muziki (be sung a cappella) au kwa kutumia
vyombo. Mwimbaji huyo kwa lugha ya ki-muziki anaitwa vocalist. Ikumbukwe kuwa
pia katika vikundi vya uimbaji wapo wale wanaoongoza wengine katika uimbaji (A lead
singer) na wengine kazi yao ni kuitikia (backing singers)
N.B
Mwanadamu yeyote
mwenye uwezo wa kuongea, anauwezo wa kuimba pia.
Kama vile tulivyo na ala za aina mbalimbali, mwimbaji naye pia anazo ala
mbili muhimu:
Mdomo
wenye uwezo wa kutoa sauti ya uimbaji
Mwili
Kumbuka moja ya
vitu vya msingi katika uimbaji ni nguvu (energy)
Mckinney alisema: “As
you sing higher, you must need more energy, as you sing lower, you must
useless; as you sing higher, you must
use more space; asa you sing lower, youmust need use less””. Inamaanisha
kadri unavyotumia sana sauti hasa kwa sauti ya juu sana, ndipo unapohitaji pia
nguvu kubwa, japo wapo watu kwasababu ya uzoefu wa kuimba kwa muda mrefu au
kupitia madarasa kama yale yanayofundishwa na mwalimu John Shabani, kwo kuimba
sauti ya juu au ya chini ni jambo la kawaida.
Zipo nguvu za kiroho na za kimwili. Ili kuwa
na nguvu za kimwili unahitaji maji ya kutosha, chakula kizuri, hewa pamoja
na mazoezi ya viungo maalum kwaajili ya uimbaji au ya pumzi.
Mwimbaji pia
anahitaji Pumzi ya kutosha (Breathing support), chakula kizuri na maji ya
kutosha
Funguo (Keys) 7 za muziki
C-do, D-re, E-mi, F-fa, G-sol, A-la, B-si
Lakini kwenye skeli (scale) ziko funguo (keys)
8 : do re mi fa sol la ti do, na kila funguo ina ngazi 8. Hivyo kwa mafunzo ya
sauti kila key inawezakuwa do. Chamsingi usiimbe flat, sauti yako iwe na nguvu
(strong on key), isiwe dhaifu (weak).
Tunaipata key kwa njia mbili: wewe mwenyewe
kujitafutia au kusaidiwa na chombo cha muziki. Wewe mwenyewe ukijipa key,
waweza kubadili, lakini ukipewa key na chombo huwezi kwenda kinyume.
Hakuna wimbo unaweza kuimbwa katika funguo
zote saba, bali ufunguo (key) 1 moja ye mabadiliko ya ngazi kadhaa kati ya hizo
8. Ninaposhuka key ninaita hiyo ni flat na nikipanda chumba hiyo ni sharp,
lakini key E na B hazina sharp. Tofauti ya key moja kwenda key nyingine ni
vyumba viwili unapokuwa unatumia vyomvo vya muziki.
Kuimba kwenye tempo ni kuimba kwa kufuata mapigo ya drum au aina yoyote
ya ngoma au mshindo
Ikiwa mwimbaji hajajua kuimbia
kwenye funguo (key) na mapigo au mdundo
(beat) bado huyo anatatizo kubwa. Hakuna muziki wa zamani na wa sasa, isipokuwa
nyimbo ndio zinaweza kuwa za zamani.
MAADHI YA MUZIKI DUNIANI
Tunaposema maadhi tuna maanisha mtindo fulani wa muziki au uimbaji.
Kuna maadhi ya aina nyingi duniani, yapo maadhi ya Nchi, maadhi ya
Kabila maadhi ya Dini, maadhi ya koo n.k
Ili unielewe vizuri hapo chini ni maadhi kadhaa:
Rumba, Reggae, chakacha, kwela, kwaito, Sukous, sebene, rock, pop n.k
Sauti ni mlio wa chochote kinachoweza kusikika
SIFA ZAKUWA MWIMBAJI BORA
Sauti, kwenda na mapigo na kusimama kwenye ufunguo (Key),
mwonekano, (appearance), Uwezo wa
kuitumia sauti na kuitawala (Manage your vocal), Stage presence (Muonekano
jukwaani), kujiamini, kujitambua, kujithamini Self Cofidance), kuwa na sikio la
muziki, kuwa mbunifu na kujitengenezea swaga zako binafsi huku zinazoendana na
muonekano wako usoni na mwili mzima. n.k.
HATUA 4 ZA KUREKODI AU KUWA NA ALBAM BORA
1.
Mwimbaji kuwa bora
2.
Tungo au ujumbe bora
3.
Muziki bora
4.
Studio bora
NGUZO
4 ZA MUZIKI
1.
Kusikiliza muziki/uimbaji (Listening)
2.
Kuhifadhi muziki/uimbaji (Copying)
3.
Kuiga au kukariri (meditate)
4.
Kuzalisha muziki (producing)
Mazoezi kwa mwimbaji
Yapo
mazoezi maalum kwaajili ya kuboresha uimbaji na pia kumfanya mwimbaji awe na
ngu ya kutosha na kuepukana na baadhi ya magonjwa. Kwa ushauri zaidi wasiliana
na mwalimu John Shabani.
Pamoja na faida
nyingi za mazoezi lakini pia mazoezi huchangamsha mwili, hulainisha koo,
husaidia kuwa na pumzi ya kutosha, hukuhepusha au kupunguza baadhi ya magonjwa
kama kisukari, presha n.k, hung’arisha ngozi, na kusaidia mfumo wa mzunguko wa
damu, mazoezi husaidia katika mfumo wa usagaji chakula kuwa mzuri , kukupa
nguvu na kuweza kufanya kazi kwa nguvu zako bila kujiskia umechoka na mwisho wa
siku hupunguza mafuta mwilini, hupunguza
uzito, kunyoosha na kuimarisha misuli ya mwili, husaidia mapigo mazuri ya moyo
kwa kuongeza kasi ya mapigo yake wakati wa mazoezi, unguza mrundiko wa damu
kwenye mishipa, hii ni muhimu kwa sababu mgando wa damu husababisha magonjwa ya
moyo pamoja na kupoteza fahamu, mazoezi huimarisha mifupa ya mwili, huboresha
usingizi ambao unafaida sana kwa mwimbaji.
Tafadhali, inawezekana lugha niliyoitumia hujaielewa sana, nawakati mwingine
nimechanganya na kingereza au lugha ya muziki. Ikumbukwe kuwa muziki una lugha
yake, na pia nimejaribu kutafsi kutoka kwenye notisi zangu ambazo mimi mwenyewe
najifunza kwa lugha ya kingereza. Lakini kwa ushauri zaidi tuwasiliane.
Kumbuka muziki au uimbaji ni kama bahari, kila mtu anaogelea pale
anaweza kufiki, mimi naweza nikakutoa hapa nikakupeleka pale, na mwingine
akakutoa pale na kukupeleka kwingine. Hakuna aliyefika kikomo cha kujua muziki
au uimbaji, sote ni wanafunzi, na pia katika kufundishana sote tunajifunza.
Ikiwa unataka kuwa mwimbaji bora, na unahisi bado unatatizo fulani
tuwasiliane.
Jinsi ya kuponya na kutunza Sauti yako
- Fanya mazoezi ya pumzi kadiri uwezavyo
- Kunywa maji ya moto kadiri uwezavyo
- Epuka kupaza sauti au kupayukapayuka bila mpangilio
- Pia mvuke wa maji yaliochemsha husaidia
John Shabani akiongoza sifa
Moja ya huduma za John Shabani
Marehemu Debora shabani akihudumu
Mwalimu John akiongoza mazoezi yapumzi
Joyce John akijifunza kupiga kinanda
MAFUNZO YA SAUTI
VOCAL TRAINING
By John Shabani
Mobile: 0716560094, 0754818767
Facebook: John Shabani
Mambo ya msingi yanayofunzishwa katika program hii:
Ø
Historia
ya uimbaji
Ø
Tofauti
ya mwimbaji na mwanamuziki
Ø
Vyakula
na vinywaji vinavyofaa na visivyofaa
Ø
Sifa
na mbinu za kuwa mwimbaji bora
Ø
Jinsi
ya kuitunza na kuiponya sauti yako
Ø
Amri
10 za sauti
Ø
Matumizi
ya kipaza sauti (Microphone technique)
Ø
Utunzi
wa nyimbo
Ø
Mazoezi
ya viungo yanayofaa kwa mwimbaji na faida zake
Ø
Ushauri
kwa wanaotaka kurekodi nyimbo
Kuimba
ni kutamka maneno katika hali ya ki-muziki au pia twaweza kusema ni kutamka
maneno moja baada ya jingine kwa sauti yenye lahani (sauti ya ala ya muziki,
tuni) au ghani
Kama vile tulivyo na ala za aina mbalimbali, mwimbaji naye
pia anazo ala mbili muhimu:
·
Mdomo wenye uwezo wa kutoa sauti ya
uimbaji
·
Mwili
Kumbuka
moja ya vitu vya msingi katika uimbaji ni nguvu (energy) “As you sing
higher, you must need more energy, as you sing lower, you must useless”.
Zipo nguvu za kiroho na za kimwili. Ili kuwa na nguvu za kimwili unahitaji maji
ya kutosha, chakula kizuri pamoja na mazoezi ya viungo.
MAZOEZI NA FAIDA ZAKE
Fikiria mwenyewe kama mwanamichezo au mtu wa fani fulani na
jifunze kuwa mtu wa kula na kunywa kulingana na fani yako: Aina ya chakula na
kinywaji na muda wa kutumia ni jambo la
kuzingatia sana. Kula na kunywa ni muhimu lakini Jiepushe na ulafi kwani huleta
uchovu, mfumo wa kupumua kuathirika na wakati mwingine kusababisha magonjwa.
Kuna
misimu fulani kama msimu wa vumbi au baridi kali au alegi au matatizo mengine
kibao, wakati mwingine aina fulani ya dawa kwa ajili ya ugonjwa fulani, Wakati
mwingine husababisha mafua au kutokwa na kamasi mara kwa mara au kukausha koo
kabisa, hivyo husumbua sana na kuathiri mfumo wako wa kuimba. Wakati mwingine
mazingira ya shughuli au kazi tuzifanyazo au pia mazingira ya makazi huweza
kuathiri sauti zetu. Hivyo masomo ya utunzaji wa sauti ni ya muhimu sana.
Vilaji na vinjywaji visivyofaa Kabla ya kuimba
Vilaji na vinjywaji visivyofaa Kabla ya kuimba
Kuhusu chakula, ni muhimu ili kuepuka kuimba tumbo likuwatupu kabisa. Kuimba ni kama
riadha, inahitajika nguvu kwa ajili ya utendaji wako. Hata hivyo, ni muhimu pia
kuepuka kuimba tumbo likiwa limeshiba sana. Yapo madhara mengi yanayotokana na
shibe. Unaweza ukawasiliana na mwalimu wa sauti ili kujua madhara hayo. Kumbuka
kuimba ni kazi ngumu, unahitaji mafuta (you need fuel), hivyo inashauriwa kuwa
na mlo wa kawaida wa saa moja au mbili kabla ya uimbaji ni bora zaidi.
Kulingana na mazoea yetu vipo vyakula na vinywaji ambavyo ni
vigumu kuachana navyo ghafla, mengine huchukua muda. Lakini hata hivyo kwa
ajili ya kutunza koo (Mashine inayozalisha sauti) pamoja na kujihepusha na
madhara yanayoweza kujitokeza unapokuwa na shughuli nzito ya uimbaji, ni muhimu
ujihepushe navyo. Nitakuambia kwa ufupi kuhusu vyakula visivyofaha unapokuwa na
shughuli za uimbaji. Kwasababu za msingi si rahisi kukutajia kwa undani madhara
ya baadhi ya vyakula au vinywaji, wasiliana na mwalimu kwa wakati wako.
Baadhi ya vyakula na vinywaji vya kuepuka kabla ya kuimba ni
kama vile:
- Vinavyoleta mwasho au kukera koo (throat irritants): vyakula au vinywaji vinavyochangamsha, kusisimua au kulewesha (Overly spicy foods) , kama vile kahawa na pilipili, vinywaji baridi sana, sukari iliyosafishwa, chocolate.
- Jamii ya vitu vyenye alkoholi, Sigara, tumbako, bangi, ugoro na aina yoyote ya madawa ya kulevya
·
Vyakula vinavyoongeza mucous (sehemu
ya kiwambo cha seli inayozunguka mfereji wa chakula): maziwa, koni,
malai/maziwa yenye ubarafu (ice cream), maziwa mgando na aina nyingine ya
maziwa (dairy products)
- Vyakula vinavyofanya koo kuwa kavu: matunda jamii ya machungwa, pombe
- Soda na aina ya vinywaji vinavyochemsha au vinavyojaza gesi au hewa katika tumbo
- Vyenye ubaridi sana au barafu: husababisha koo kubana, kuminywa au kunyongwa.
·
Vyakula vinywaji
vyenye ubarafu na pombe (ikiwa ni pamoja na mvinyo na bia). Kuna baadhi ya watu
pia huwa na alegi (kwa mfano, baadhi ya waimbaji wana shida na matunda jamii ya
machungwa, ngano, karanga, samakigamba au soya).
·
Vyakula vyenye mafuta mengi
Ili kuwa na afya nzuri katika mwili na
katika uimbaji wako zingatia :
·
Punguza matumizi mengi ya sukari, ongeza matumizi ya
matunda
·
Punguza kula
nyama nyekundu, ongeza matumizi ya mbogamboga
·
Punguza matumizi
ya soda, ongeza matumizi ya maji
·
Punguza
kuendesha, ongeza kutembea kwa miguu
·
Punguza
kupoteza muda wa kulala, Zingatia kulala kwa wakati
·
Punguza msongo
wa mawazo, ongeza kupumzika
Zingatia :
·
Maji ya moto au
aina ya chai mitishamba (herbal tea) ni bora, Mwimbaji mzuri hutumia class 8 za maji kwa siku,
wapo ambao hutumia hadi lita 4 pia yapo maji ya ziada kutoka katika vyakula.
·
Kupasha sauti kwa kukohowa kohowa
sio njia ya kukusaidia kuimba vizuri, badala yake
hukata sauti
·
Pamoja na umuhimu wa maji, lakini acha
matumizi ya maji mengi saa moja au mbili kabla ya kuanza uimbaji badala yake
asali ni bora zaidi. Lakini pia sauti ikipatwa na tatito unaruhusiwa kupata
maji ya moto pamoja na asali
·
Angalizo kuhusu mazoezi: Mazoezi huwa yana ugumu
wake hasa pale unapokuwa unaanza, usikate tamaa wala usikubali uvivu au maumivu
yakakurudisha nyuma. Jitengee muda maalum kwa ajili ya kufanya mazoezi na
usianze kwa kufanya mazoezi magumu bali anza na mepesi mepesi ili kuupa mwili
nafasi ya ku-adopt mabadiliko
koo hupendezwa, hutulizwa, huburudishwa, hutengenezwa na:
Aina fulani ya pipi, asali, mvuke,
chai fulani ya mitishamba au mchaichai, kusafisha koo kwa maji chumvi, baadhi
ya dawa kwa ushauri wa daktari n.k
Jinsi ya kulinda na kuiponya Sauti yako
Kila mtu anawezakuitumia sauti yake, lakini si
kila mtu anajua jinsi ya kuitunza au kuiponya inapopatwa na tatizo. afya yake,
au nini cha kufanya wakati si tu kufanya kazi haki. Makala hii itasaidia kila mtu kujifunza jinsi ya kuponya
sauti na pia kutoa ushauri wa jinsi ya
kuitunza na kuifanya kuwa na afya na nguvu kwa ajili ya siku zijazo
Masomo
haya yanawafaha walimu, wainjilisti, wanasiasa, wazazi, wanasheria, madaktari,
na waimbaji, na kila mtu ambaye shughuli zake hulazimi kakuongea sana.
·
Kama sauti yako imejeruhiwa
vibaya, basi jambo muhimu zaidi la kufanya sasa hivi ni kuacha kutumia hiyo
Sauti, ipumzishe. Punguza pia kuzungumza kwa muda mrefu na hasa kwa
kupaza sauti kubwa na kutumia muda kidogo zaidi katika
ukimya.
·
Jambo jingine kubwa ambayo husaidia sauti iliyojeruhiwa ni chai ya moto
(Kama vile coat tea). Unaweza kupata pia
dawa za mitishamba zilizohifadhiwa kitaalam katika maduka ya dawa,
lakini ikiwa dini yako au tamaduni yako haina shida katika hili. Kunywa angalau kikombe asubuhi na kikombe wakati wa usiku.
·
kama kuna kitu ambacho kinaweza kusaidia kuponya sauti yako na pia
inaweza kutumika kulinda kwa haraka ni
unywaji wa maji ya kila siku. Maji husaidia na sauti yako katika afya nzuri
TANGAZO:
TANGAZO:
Darasa hili la sauti na uimbaji linaendelea, njoo darasani, utajifunza mengi zaidi.
Piga simu namba 0713778778 na 0754818767 ili upewe maelekezo ya tunapopatikana na muda wa darasa.
Subscribe to:
Posts (Atom)
HEART OF WORSHIP
MEET WITH JOHN SHABANI
FUTA MACHOZI By John Shabani
Google+ Badge
MTOTO WA MFALME (THE KING'S SON) By John Shabani!
John Shabani (Christian Leadership University)
WHO'S JOHN SHABANI (Prince John)
LISTEN TO PRAISE POWER RADIO LIVE. 99.3 FM - DAR ES SALAAM
www.ustream.tv/channel/ppr-broadcast
ABOUT THIS BLOG
NAKUPENDA By John Shabani
WORSHIP HOUR WITH JOHN SHABANI
Pages
- Home
- WHY VISIT TANZANIA - CULTURAL TOURISM
- ONGEZA KIPATO NA ORIFLAME - INCREASE YOUR INCOME WITH ORIFLAME
- AFRICAN GOSPEL SINGERS (PHOTOS & HISTORY)
- INTERNATIONAL GREAT SERVANTS OF GOD/ WATUMISHI WAKUU WA MUNGU DUNIANI
- GREAT AFRICAN PASTORS, EVANGELISTS & TEACHERS - WATUMISHI WAKUU WA MUNGU AFRIKA
- CHRISTIAN TEACHINGS (MASOMO MBALIMBALI) (ENGLISH AND SHAHILI MESSAGES FROM DIFFERENT PREACHERS OF THE GOSPEL)
- JOHN SHABANI WITH THE MISSION OF RAISING TALENTS
- VOCAL TRAINING - DARASA LA UIMBAJI
- JOHN SHABANI AND HOPE TRUST “To bring hope to the Children and Youth”
- ABOUT JOHN SHABANI AND THIS BLOG (MADHUMUNI YA BLOGU NA HISTORIA YA MMILIKI)
- HEALTH TIPS - AFYA
- JOHN SHABANI PHOTO GALLERY
- JOHN SHABANI AND DISADVANTAGED CHILDREN
- JOHN SHABANI - NEW ALBUM
- AFRICA (BANDS AND CHOIRS) KWAYA NA BAND ZA AFRIKA
- AFRICAN BISHOPS, PASTORS AND EVANGELISTS (Ministries & Contacts)
- SWAHILI PRAISE AND WORSHIP SONG LIST
- CONTACT US - TWASILIANE
- JOHN SHABANI ( PRAISE AND WORSHIP MINISTRY)
CONTACT US
Would you like to become a partner with John Shabani Ministry & this blog,
please contact us:
E- mail: touchingvoice@yahoo.com or
princejohntz@yahoo.com
Mob: +255 754 818 767 or +255 716 560 094
please contact us:
E- mail: touchingvoice@yahoo.com or
princejohntz@yahoo.com
Mob: +255 754 818 767 or +255 716 560 094
www.facebook.com/john.shabani
FOLLOW ME ON FACEBOOK
OTHER BLOGS & WEBSITE ( BLOG NYINGINE)
- Gospel News Media
- EAST AFRICAN GOSPEL
- KENYA GOSPEL ARTISTS
- AFRICAN PASTORS
- CHOPAMCHOPANGA
- RAY THE GREATEST
- MAINDA SMALL BABY
- RUMAFRICA
- ROSE MUHANDO
- Krystaal
- JIJI LA DAR KATIKA PICHA
- http://rumatz.com
- AFRICA MUSIC AWARD
- Haki za Wanamuziki
- MILLARD AYO
- SAMWELI SASALI
- EV. MUNISHI
- BADOO
- Lady Jay Dee
- Strictly Gospel
- NYIMBO ZA INJILI
- MICHUZI
- KABULA J.GEORGE
We welcome your comments suggestions and support. Please, mention your e-mail address)
TANZANIA GOSPEL ALL STARS
-
MARUFUKU KUKATA TAMAA N ever ever give up John Stephen Shabani P. O. BOX 15155 Dar es salaam, Cell: ...
-
WOMENS OR GIRLS Marehemu Anjela Chibalonza Angela Chibalonza Runiga was born on Novem...
-
Born in Kigoma Tanzania mid days of November to a born again Christian family and had a religious upbringing. At age of 15 yea...
-
Rev. Lucy Natasha with his mother Dr. Rev. Esther Wanjiru "Natasha is the founder and visionary of prophetic latter glory Ministr...
-
Staa wa muziki wa Gospel Tanzania Martha Mwaipaja hatimae ameolewa, pembeni yake ni mumewe Pastor John Said. Martha Mwaipaja ambae ni mion...
-
KUSIFU NA KUABUDU (Zaburi 147:1, 32,:1, 48:1, 96:4, 2nyakati 5:11-14, Yohana 4:20-23) Kua...
-
Hii ndio kwaya maarufu ya Ambassadors of Christ ya Remela/Rwanda Hii nd...
-
An Independent Spiritual, Religious, Non Governmental Organization Efatha Ministry began in Tanzania with servant of God who is a...
-
SINGING COURSE (Darasa la uimbaji) WITH Prince John Shabani Table of contents · Introduction · Singing · ...
-
Ni maelezo mbalimbali kuhusu maisha ya Akofu. Baada ya kuulizwa maswali mbalimbali kuhusu maisha yake na huduma, hapa Askofu Zakaria ...
ROBERT KAYANJA MINISTRIES - www.kayanja.org
IDADI YA WATU WANAOTEMBELEA
625794
JOHN SHABANI AND HOPE TRUST “Bringing hope to the Children & Youth”
“To bring hope to the Children and Youth”
Followers
FOLLOW ME ON TWITTER
John Shaban. Powered by Blogger.
Copyright © 2011 GOSPEL IN AFRICA | Powered by Blogger
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Buy DigitalOcean Accounts
JibuFutahttps://shopvcc.net/product/buy-amazon-aws-accounts/