MAKALA:NANI ANAFUATA TANZANIA?
NANI ANAFUATA TANZANIA? Na Ev Mhugo Hantish Kutoka nchini Atlanta, Georgia Gospel Headlines Leo imekuletea mwimbaji mwenye karama ya ajabu na ya pekee katika kumwinua na kumtukuza Mungu aliye hai, Dr. Sonnie Badu. Huyu ni mwimbaji, mchungaji wa kanisa la Rock Hill alilolianzisha mwenyewe mwanzoni mwa 2017 nchini humo. Amejikita zaidi katika uimbaji wa nyimbo za injili kwa namna ya 'Live Concert' ambayo imekuwa ikifanyika baraka sana mioyoni mwa watu waliobahatika kuhudhuria baadhi ya matamasha yake. Leo katika moja ya posts alizo post kupitia mtandao wa instagram akiwa Marekani ni picha iliyoonyesha baadhi ya tuzo na medani alizozipata kwa njia ya huduma yake. Picha hiyo ilipewa Caption ifuatayo "you will not labour in vein. God will honor you before the year ends...look up to jesus " yakiwa na maana "hautafanya kazi patupu. Mungu atakuheshimisha kabla ya mwaka kuisha.... wewe mtazame Yesu" Picha hiyo imemwoyesha ak...