GHL On Pre Sunday: MAJIBU YA PADRE KWA MUUMINI WAKE.
Mwanamke mmoja alimwendea Padre na kumwambia..."Sitaendelea kuja Kanisani..." Padre akamuuliza, unaweza kuniambia kwa nini unasema hivyo? Yule mwanamke akasema, "wakati wa ibada naona watu wakiwa wanatumia simu zao, wengine wakisengenya, wengine nao hawaishi ipasavyo kama Wakristo. Wote ni wanafiki tu." Padre akakaa kimya. Kisha akamjibu yule mama, Sawa...Lakini nikuombe unifanyie jambo moja kabla hujafanya maamuzi? Mwanamke akaitikia, "jambo gani hilo?" Padre akamwambia, "chukua glasi ya maji na ulizunguke Kanisa mara mbili ukiwa nayo mkononi, na uhakikishe kwamba hakuna hata tone la maji linalodondoka." Mwanamke akasema...."hilo naliweza kabisa!" Akazunguka Kanisa mara mbili akiwa na ile glasi ya maji na akamrudia Padre na kumwambia kwamba, "nimekamilisha." Baada ya kuona vile, Padre akamuuliza maswali matatu: 1. Uliona mtu yeyote akiwa anatumia simu yake? 2. Uliona mtu yeyote akiwa anasengenya? 3. Je, uliweza kumwona mtu ye...