Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari, 2017

TOFAUTI YA NEEMA NA REHEMA

Picha
Ev. Mhugo Hantish Mhugo Hantish at Africa/Dar_es_Salaam . 11 hrs · Instagram · Si kwa sababu ya NEEMA aa Ila ni kwa sababu ya REHEMA za Mungu ndizo zilizonifanya kukutana na NEEMA ya WOKOVU WA MUNGU. # SIDHANIkamaNIMEELEWEKAvizuri

ACHA MAZOEA YA IBADA.

BWANA YESU ASIFIWE! LEO NIMEONA TUJIKUMBUSHE KIDOGO HABARI ZA IBADANI. TUSOME KWANZA KATIKA BIBLIA YETU TAKATIFU.  MITHALI 7:1-2 "Mwanangu, yashike maneno yangu, Na kuziweka amri zangu akiba kwako. Uzishike amri zangu ukaishi, Na sheria yangu kama mboni ya jicho lako"   Haleluya! Namshukuru sana Mungu mwenye rehema ya kwamba ameniwezesha kuiona siku hii na kuitumia kwa misingi aliyoniachia tangu kuzaliwa kwangu. Nimeona nizungumze nawe maneno haya leo mbele yako. namsihi Roho wa Bwana akutangulie katika kulielewa neno hili.   Huku nikiendelea, anza kufikiri maisha yako ni mara ngapi umehudhuria ibadani huku ukiwa na fahamu za kutosha? katika siku au ibada zote ulizokwisha kuhudhuria umepiga hatua ya kiroho kwenda mbele zaidi?  nauliza swali hi kwasababu wapo watu humu au nje ya ibadani ambao wao kazi yao kila jumapili wanaleta mahudhurio tu kwa mchungaji, lakini mioyoni mwao hawamjui Mungu na wala hawana mpango wa kumpokea Mungu nafsini mwao. Wao wakiingia mal...

EV MHUGO HANTISH WITH FARIDA HANTISH tar 14.02.2017

Picha
VIDEO : jinsi ilivyokuwa tar 14.02.2017 kwa akina Hantish na Farida. Yamkini ndoa yako ina misukosuko, Hadi unatamani uachane na mume/mke wako, (kwa wale wenye furaha na amani hii haiwahusu) Au unafikia hatua ya kutaka kujiua, au kumuua, TAMBUA ya kwamba Roho wa Mungu yu upande wako... Atakusimamia, atakutetea... Wewe mwenye mpango mkakati wa kuoa au kuolewa... Tulia kwa makini kabisa mbele za Mungu na kumwomba akuchagulie kilicho chema kabisa. # usikurupuke Leo wanasema ni siku ya WAPENDANAO, je ina maana siku zingine zote ni siku za WACHUKIANAO? Siku hii isikufanye wewe utende dhambi, isikufanye umtendeshe dhambi mwingine. # jichunge na # jihadhari ...  MUNGU AMEAGIZA UPENDO WA KWELI.. UPENDO WA KWELI HAUFI, HAUJI NA KUONDOKA, WALA KUPOTEA... # MUNGU AKUBARIKI WEWE PAMOJA NA JAMAA ZAKO. .  

MUULIZE MUNGU "NIIMBE NINI?"-MCH. ABIUD MISHOLI.

Picha
Ev. Mhugo Hantish (kushoto)akiwa na Mch. Abiud Misholi(kulia ) MAKALA:   UIMBAJI ULIOBARIKIWA NA MUNGU  Inawezekana kabisa wewe ni miongoni mwa watu wengi wanaomfuatilia sana kwa karibu Mchungaji Abiud Misholi pamoja na nyimbo zake ambazo zimekuwa zikifanyika faraja kwa watu wenye shida mbalimbali. kwa wewe uliyehudhuria baadhi ya matukio ya huzuni kama vile misiba bila shaka umeshuhudia nyimbo za Mtumishi huyu zikitumika sana pengine kuliko zingine.    www.hantishmhugo.blogspot.com ilitamani kufahamu mengi kuhusu huduma yake kwa ujumla. Ikafanikiwa kukaa naye meza moja Kanisani kwake lililopo mjini Mbeya kitalu T(block T). Jambo la kwanza blog ilitamani kujua kwanini Mchungaji amekua akiimba nyimbo za huzuni na mara nyingi zimekua zikitupitisha wengi katika maisha magumu halisia. Kwa ufupi kabisa aliweza kujibu kwamba si kwa akili zake bali humuuliza Mungu katika sala kwamba aimbe nini. kwanza lazima uketi kwa unyenyevu mbele za Mungu na kumwomba ki...

Neno: Bibilia Takatifu

Wagalatia 5:22-23 Neno: Bibilia Takatifu (SNT) 22  Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumili vu, wema, fadhili, uaminifu, 23  upole, kiasi. Hakuna sheria inayopinga mambo kama haya. Neno: Bibilia Takatifu (SNT) Copyright © 1989 by Biblica

Habari:Umoja wa waimbaji_Mkoa wa Mbeya umesaidia ufanisi wa huduma ya uimbaji.

Picha
HABARI Na Mwandishi wetu. MBEYA: Ili kukuza na kuitangaza huduma ya uimbaji kwa haraka na kwa mafanikio chanya pasipo kuathiri kusudi la Mungu waimbaji  wa nyimbo za Injili kutoka mkoa wa Mbeya wameamua na wamekubaliana kuunda chombo cha pamoja kiitwacho (OMGS)-ORGANIZATION OF MBEYA GOSPEL SINGERS chenye lengo la kusaidiana kwa karibu baina ya waimbaji katika huduma hiyo ya uimbaji.   Akiongea kwa umakini mkubwa wakati wa mahubiri katika mkutano wa ndani uliowakutanisha waimbaji na waumini wote kwenye Kanisa la EAGT kwa Mchungaji Mbena, Mwenye kiti wa UMOJA huo alisema "mwaka 2017 lazima uwe ni mwaka wa mafanikio makubwa kwetu katika huduma hii ya uimbaji". Aliendelea mbele zaidi na kusema "... nasema kama nabii kwamba baada ya mikutano hii kuisha tutarajie kuona kila mwimbaji anapokea simu nyingi za mialiko hadi nje ya nchi kama Kenya n.k. na wala hatutashangaa maana tumeshapewa kibali.."   Naye Katibu wa umoja huo Bw. Mwansasu alipokua akizungumza n...