Habari:Umoja wa waimbaji_Mkoa wa Mbeya umesaidia ufanisi wa huduma ya uimbaji.


Image may contain: one or more people, people standing and indoor

HABARI

Na Mwandishi wetu.

MBEYA:

Ili kukuza na kuitangaza huduma ya uimbaji kwa haraka na kwa mafanikio chanya pasipo kuathiri kusudi la Mungu waimbaji  wa nyimbo za Injili kutoka mkoa wa Mbeya wameamua na wamekubaliana kuunda chombo cha pamoja kiitwacho (OMGS)-ORGANIZATION OF MBEYA GOSPEL SINGERS chenye lengo la kusaidiana kwa karibu baina ya waimbaji katika huduma hiyo ya uimbaji.
  Akiongea kwa umakini mkubwa wakati wa mahubiri katika mkutano wa ndani uliowakutanisha waimbaji na waumini wote kwenye Kanisa la EAGT kwa Mchungaji Mbena, Mwenye kiti wa UMOJA huo alisema "mwaka 2017 lazima uwe ni mwaka wa mafanikio makubwa kwetu katika huduma hii ya uimbaji". Aliendelea mbele zaidi na kusema "... nasema kama nabii kwamba baada ya mikutano hii kuisha tutarajie kuona kila mwimbaji anapokea simu nyingi za mialiko hadi nje ya nchi kama Kenya n.k. na wala hatutashangaa maana tumeshapewa kibali.."
  Naye Katibu wa umoja huo Bw. Mwansasu alipokua akizungumza na www.hantishmhugo.blogspot.com alisema kuwa mara baada ya kumaliza ziara ya mikutano ya kila wilaya utaandaliwa mkutano mkuu katikati ya jiji la mbeya mnamo mwezi wa 10(tarehe bado haijatajwa) ambapo watu watazamie kupokea na kushudia mapinduzi makubwa kwenye huduma hii ya Muziki wa injili.
  Ratiba ya mikutano tayari imeshapangwa kwa mfurulizo wa mwaka mzima ambapo kufikia mwezi wa 10 itakua imekamilika na imetosha kuzunguka karibu kila Wilaya ndani ya mkoa wa Mbeya ambapo wilaya ya Mbarali imeshateembelewa tar 27-30/01/2017. 
  Katika Mkutano huo uliofanyika mjini Mbarali ulihudhuriwa pia na waimbaji wageni mbali mbali ambao nao walifanikiwa kujiunga kwenye Umoja huo. 
 Akitoa baraka za Mungu kwa waimbaji, Mchungaji Mbena alisisitiza waimbaji kuwa wanyenyekevu sana maana ndio siri ya kufanikiwa kwao na Mungu atawakweza kwa wakati wake. "..lakini pamoja na mipango hii mliyo nayo, nawasihi sana jambo la muhimu ..{unyenyekevu} ndio silaha ya mafanikio" alisema.


HAPA CHINI NIMEKUWEKEA VIDEO NDOGO UIONE JINSI WAIMBAJI PAMOJA NA WAUMINI WENGINE WALIVYOSHUKIWA NA WINGU LA SIFA.....ITAZAME



LikeShow more reactions
Comment

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

SOMO:KUSIFU NA KUABUDU KATIKA BIBLIA.

HISTORIA YA MITUME WA YESU KRISTO NA VIFO VIFO

SOMO: MAONO NA NDOTO