MUULIZE MUNGU "NIIMBE NINI?"-MCH. ABIUD MISHOLI.

Ev. Mhugo Hantish (kushoto)akiwa na Mch. Abiud Misholi(kulia)

MAKALA:  

UIMBAJI ULIOBARIKIWA NA MUNGU

 Inawezekana kabisa wewe ni miongoni mwa watu wengi wanaomfuatilia sana kwa karibu Mchungaji Abiud Misholi pamoja na nyimbo zake ambazo zimekuwa zikifanyika faraja kwa watu wenye shida mbalimbali. kwa wewe uliyehudhuria baadhi ya matukio ya huzuni kama vile misiba bila shaka umeshuhudia nyimbo za Mtumishi huyu zikitumika sana pengine kuliko zingine. 
  www.hantishmhugo.blogspot.com ilitamani kufahamu mengi kuhusu huduma yake kwa ujumla. Ikafanikiwa kukaa naye meza moja Kanisani kwake lililopo mjini Mbeya kitalu T(block T). Jambo la kwanza blog ilitamani kujua kwanini Mchungaji amekua akiimba nyimbo za huzuni na mara nyingi zimekua zikitupitisha wengi katika maisha magumu halisia. Kwa ufupi kabisa aliweza kujibu kwamba si kwa akili zake bali humuuliza Mungu katika sala kwamba aimbe nini.
kwanza lazima uketi kwa unyenyevu mbele za Mungu na kumwomba kibali cha wewe kufanya huduma yoyote ile katika ROHO. Kisha ukishapokea kibali sasa ni nafasi nyingine (kama ni mwimbaji) usikurupuke tu na kuingia studio, "mwulize Mungu Niimbe nini?" au niimbe nyimbo za namna gani. Mimi nilipokwisha fanya hivyo nikaambiwa ninatakiwa kuwafariji watu wenye shida na matatizo, natakiwa kuwatia moyo. Sikusita tena, nikatii na kunyanyuka kulitimiza kusudi lake Mungu.-Mchungaji Abiud Misholi.
Aliendelea mbele zaidi na kusema "kuna watu wameambiwa waimbe nyimbo za mahubiri, nyimbo za sifa, za kuabudu. Wote hao ni makusudi yake Mungu"

Kwa habari nyingine tu ni kwamba hivi sasa Mchungaji Abiud anamiliki bendi iitwayo FARAJA BEND.

   Ndugu yangu, nimeona nikushirikishe habari hii ili kusudi kwa yeyote mwenye ndoto au anayetaka kuimba lazima azungumze na Mungu wake kwanza chumbani mwake. Ili hata nyimbo ziweze kuwabariki wengi mahali pengi nchini na hata nje ya nchi yetu ya Tanzania. Hata kama wewe mwenye wimbo hutafika marekani lakini wimbo utakutangulia kwenda kuhubiri injili.
 

Ev Mhugo Hantish akiwa kwenye mkutano wa ndani wa waimbaji-Mbeya



TANGAZO 
JE, UNAHITAJI KUJIFUNZA KUPIGA KINANDA?
UNHITAJI KUJUA NAMNA YA KUIMBA KWA USTADI?
UNAHITAJI KUJUA NAMNA YA KUITUNZA SUTI YAKO KIAFYA?
WASILIANA NASI KWA NAMBA 0768788303 AU TUTUMIE EMAIL hantishmhugo@gmail.com
TUTAKUSAIDIA HAYO NA MENGINE MENGI KUHUSU UIMBAJI MZURI.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

SOMO:KUSIFU NA KUABUDU KATIKA BIBLIA.

HISTORIA YA MITUME WA YESU KRISTO NA VIFO VIFO

SOMO: MAONO NA NDOTO