ACHA MAZOEA YA IBADA.

BWANA YESU ASIFIWE!
LEO NIMEONA TUJIKUMBUSHE KIDOGO HABARI ZA IBADANI. TUSOME KWANZA KATIKA BIBLIA YETU TAKATIFU.
 MITHALI 7:1-2
"Mwanangu, yashike maneno yangu, Na kuziweka amri zangu akiba kwako. Uzishike amri zangu ukaishi, Na sheria yangu kama mboni ya jicho lako"
  Haleluya!
Namshukuru sana Mungu mwenye rehema ya kwamba ameniwezesha kuiona siku hii na kuitumia kwa misingi aliyoniachia tangu kuzaliwa kwangu. Nimeona nizungumze nawe maneno haya leo mbele yako. namsihi Roho wa Bwana akutangulie katika kulielewa neno hili.
  Huku nikiendelea, anza kufikiri maisha yako ni mara ngapi umehudhuria ibadani huku ukiwa na fahamu za kutosha? katika siku au ibada zote ulizokwisha kuhudhuria umepiga hatua ya kiroho kwenda mbele zaidi?
 nauliza swali hi kwasababu wapo watu humu au nje ya ibadani ambao wao kazi yao kila jumapili wanaleta mahudhurio tu kwa mchungaji, lakini mioyoni mwao hawamjui Mungu na wala hawana mpango wa kumpokea Mungu nafsini mwao. Wao wakiingia malangoni na kutoka hawana hasara yoyote.
  leo Mungu anatukumbusha sasa kwa kusema MWANANGU, ikiwa sisi ni watoto wa Mungu basi hatuna sababu ya kupinga au kuenda kinyume na kusudi lake juu yetu. Mungu ametuthamini sana hadi kitendo cha kutuita wananwe. Anaposema YASHIKE MANENO YANGU anatutaka, sio anatuomba. Ikiwa angekuwa anatuomba basi angeweza tumia maneno haya NAOMBA UYASHIKE... tafsiri yake ni kwamba Mungu wetu ameyaona mazoea yetu katika kumtumikia Mungu wetu  hata anaona kama hakuna utofauti katika ya jana na leo. Tusiwe kama mti usio zaa matunda, wenyewe umekaa kihasara hasara shambani hadi Bwana shamba anatamani kuung'oa(LUKA 13: 6-9)
  Haleluya!
Wapendwa wa Mungu, tumepewa amri au sheria za Mungu ili ziwe msaada wetu katika kuenenda kwetu pasipo kumkosea Mungu. ndipi anapo sema ...NA KUZIWEKA AKIBA KWAKO AMRI ZANGU..
Sote tunajua kwamba kila mtu anaejitegemea huweka chakula gharani kama akiba ya baadae na kesho. Vivyo hivyo hata Mungu naye anasisitiza kwamba tuweke akiba ya Amri zake mioyoni mwetu. Ili tunapoendelea mbele katika misingi ile ambayo Mungu anaihitaji, iwe ni matunda ya kuishi katika kuzishika na kuzifuata Amri zake.
  Haleluya!
Dah..! mpendwa wa Mungu nikuhakikishie kwamba Mungu huyu bado anatuhitaji na ndio maana hachoki kutuasa maneno mazuri. Haya hebu fikiri angeacha kusemezana nasi kama hivi leo, Tungekuwa wapi taifa la Mungu? ni lazima tungekua tumechakaa na kuvubaa kabisa. simama na umwambie Mungu kwamba unaacha kuabudu kwa mazoea na sasa unaanza kukua kiroho.
AMEN

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

SOMO:KUSIFU NA KUABUDU KATIKA BIBLIA.

HISTORIA YA MITUME WA YESU KRISTO NA VIFO VIFO

SOMO: MAONO NA NDOTO