SOMO:NINI MAPENZI YA MUNGU JUU YAKO?
Mungu ana mapwnzi mema kwetu sisi wanadamu,yaani Mungu anatupenda zaidi. Mathayo 7:21 Luka 6:46-47 ". ..si kila mtu aniambiaye Bwana Bwana ndiye atakaye ingia katika ufalme wa Mbinguni, bali ni yeye afanyaye mapenzi ya baba yangu wa mbinguni..." Hiyo ni sauti ya mwana wa Mungu, Yesu Kristo. Baada ya kuwa na hofu juu ya imani yao waaminio, Bwana Yesu anawauliza wanafunzi kwamba " kwanini mnaniita Bwana, Bwana lakini hamyatendi nisemayo.. ?" ...anaongeza na kusema kuwa " kila mtu AJAYE kwangu na KUYASIKIA maneno yangu na KUYATENDA nitawaonyesha mfano wake. ." sasa Mapenzi ya Mungu yaani Mungu anatarajia kuwa sisi sote tukiwa kama wana wake tunapaswa kumfuata, kuyasikia na kuyatendea kazi yale yote atuagizayo. hivyo ndiyo Mungu atakavyo.huwa ninasemezana na jamaa zangu kwamba Mungu ana makusudi ya kukuweka u hai hadi leo hii. sasa ungali hai leo fikiri ni jinsi gani umepiga hatua mbele au umerudi zaidi nyuma katika kumcha Mungu? ukiona huna hata hatu...