SOMO:NINI MAPENZI YA MUNGU JUU YAKO?
Mungu ana mapwnzi mema kwetu sisi wanadamu,yaani Mungu anatupenda zaidi.
Mathayo 7:21 Luka 6:46-47
"...si kila mtu aniambiaye Bwana Bwana ndiye atakaye ingia katika ufalme wa Mbinguni, bali ni yeye afanyaye mapenzi ya baba yangu wa mbinguni..." Hiyo ni sauti ya mwana wa Mungu, Yesu Kristo.
Baada ya kuwa na hofu juu ya imani yao waaminio, Bwana Yesu anawauliza wanafunzi kwamba "kwanini mnaniita Bwana, Bwana lakini hamyatendi nisemayo..?" ...anaongeza na kusema kuwa "kila mtu AJAYE kwangu na KUYASIKIA maneno yangu na KUYATENDA nitawaonyesha mfano wake.."
sasa Mapenzi ya Mungu yaani Mungu anatarajia kuwa sisi sote tukiwa kama wana wake tunapaswa kumfuata, kuyasikia na kuyatendea kazi yale yote atuagizayo. hivyo ndiyo Mungu atakavyo.huwa ninasemezana na jamaa zangu kwamba Mungu ana makusudi ya kukuweka u hai hadi leo hii. sasa ungali hai leo fikiri ni jinsi gani umepiga hatua mbele au umerudi zaidi nyuma katika kumcha Mungu? ukiona huna hata hatua moja uliyopiga katika siku zako za usoni, hata kwa kugusa maisha ya watu wahitaji mbele yako tu jiulize nafsini mwako kuwa ni lipi kusudi la Mungu juu yako kukuweka katika Dunia hii hadi leo.
mapenzi ya Mungu ni wewe na mie kuliishi na kulitendea kazi neno lake.(Rum 2:13) kwa sababu sio wale waisikiao sheria ndio wenye haki,bali ni wale waitendao sheria ndio wenye haki.. lakini pia Yakobo 1:22 inasema "iweni watendaji wa neno, wala si wa kusikia tu..hali mkijidanganya nafsini mwenu.."
yafaa sana tuwe watendaji wa neno, maana yatufaa nini tukisema kuwa tunayo imani ilhali hatuna mateno? imani bila matendo imekufa.. Yakobo 1:14
namna ya kuliishi/kulitumikia kusudi la Mungu.
ili kulitumikia kusudi la Mungu kaitka kizazi chako ni lazima ukubali kuongozwa na Roho Mtakatifu. katika Zaburi 32:8 tunaambiwa tutaonyeshwa njia tutakayoiendea... lakini pia katika Kitabu cha Warumi 8:14 inasema "wote wanaoongozwa na Roho Mtakatifu ni wana wa Mungu.."
Hivyo mpendwa jifunze mambo makuu mawili kuhusu namna ya kutekeleza ayapendayo Mungu wetu:-
1. kumsikiliza Roho mtakatifu anavyokuongoza. na
2. kuyatendea kazi yale yote akuagizayo Mungu wetu kuoitia Roho mtakatifu..
Mungu akujalie maisha mema katika kumcha Mungu. anza na Roho Mtakatifu katika kila Mwanzo wako.
Ameni!!!!!

Maoni
Chapisha Maoni