USIWE MWEPESI WA KUKATA TAMAA
1ISAYA1:1-17
SOMO:USIWE MWEPESI WA KUKATA TAMAA
Mpendwa msomaji wangu wa blogu hii, Bwana Yesu apewe sifa? leo nimependa kushirikiana na wewe ili tuzungumze juu ya kuto kata tamaa mapema kwa yale uliyowahi kuyaomba mbele za Mungu na pengine hadi leo hujafanikiwa. Katika Biblia tunaona Elkana alikuwa na wake wawili, mmoja mkubwa Hanna na mwingine mdogo Penina ambaye pia alifanikiwa kuwa na wana lakini Hanna hakufanikiwa kuwa na wana. ilikuwa ni kwa kipindi kirefu sana Hana hakuwa na wana. alifikia kipindi Hanna alimlilia Mungu sana. ilikuwa ni vigumu kwa akili za kibinadamu kukubaliana na maumivu yale kwa muda mrefu. na pia haikuwa rahisi kuendelea kumwomba Mungu kwa muda mrefu lakini ni kwa jinsi gani imani iliyo kuwa ndani ya moyo wa Hanna mbele za Mungu.kumbuka hapa tunamtumia sana Hanna kwa kuwa ndiye aliyepita katika maisha ya vita. lakini tutambue pia umuhimu wa Penina katika maisha ya Hanna na Elikana.
Elikana aliwapenda sana wake zake hata hakufikiri kuwatenganisha. kumbuka zawadi zake alizozitoa, alizitoa kwa wake zake wote.
sasa turejee kwenye somo husika, wengi wamekuwa wakimwomba Mungu, lakini kwa kuwa na ufinyu wa imani ndani ya mioyo yao na pia kukosa imani na Mungu wanaishia kukata tamaa. mpendwa , usikate tamaa, songa mbele , endelea kumcha Mungu maana yeye yupo kwaajili ya maisha yetu. kama wewe una matatizo kama yaliyomkuta Hanna yale ya kuchelewa kupata mtoto, basi jifunze kupitia yeye.. maana yeye alifanikiwa japo kwa kuchelewa. au hata kama una matatizo mengine lakini pia maombi yako hayajasikilizwa.
Mungu aendelee kukutunza na kukutimizia kila jema uliombalo.

Maoni
Chapisha Maoni