Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari, 2018

MAHOJIANO MAALUM NA EV. MHUGO HANTISH

Picha
TAZAMA MAHOJIANO HAPA CHINI Hello mpenzi msomaji wetu wa GOSPEL HEADLINES LEO, bila shaka ukheri wa afya kabisa. Kama ilivyo  ada kukuletea habari za wainjiishaji na injili kutoka ndani na nje ya Tanzania, leo tumekusogezea karibu yako mahojiano maalum ya Ev. Mhugo Hantish akiwa na mtangazaji wa kipindi cha FARAJA YAKO, Getrude Mwakatobe wa Radio Bomba Fm 104.1 Mbeya. PICHA KWA HISANI YA HINJU ZE ONE, DH     TANGAZO JE, UNAHITAJI KUTANGAZA HABARI YAKO HAPA   www.hantishmhugo.blogspot.pe ? KAMA NI "NDIO" TUTUMIE EMAIL YAKO KWENDA   hantishmhugo@gmail.com   AU UJUMBE/PIGA/WHATSAPP 0768788303 . gospelheadline@2018 " The voice to the voiceless "

Mr. Marco Mnanago - Usilie Mama (Official Audio)

Picha
Na Mwandishi Wetu. IRINGA. Habari yako mpenzi msomaji wetu wa GOSSPEL HEADLINES LEO? Ni siku nyingine tena iliyochukua nafasi maishani mwetu ambapo leo tunamleta kwenu mwimbaji wa nyimbo za injili aitwaye Mr.MARCO MINANAGO kutoka mkoani Iringa, ambaye leo anautambulisha rasmi wimbo wake hapa GOSPEL HEADLINES LEO. Wimbo uitwao USILIE MAMA umetengenezwa katika studio za 2Star Records katika mikono bora ya mtayarishaji Kay B.    Akizungumza na GOSPEL HEADLINES LEO, Minanago amesema "wimbo huu wa USILIE MAMA umekua na maana kubwa sana kwangu kwasababu mama ni jeshi kubwa. Hivyo nimemtumia mama ili kutuwakilisha sote ya kwamba hatutakiwi kukata tamaa tupatwapo na majaribu."   Akiongeza zaidi, Mr Marco amesema "hakuna haja ya kulia hadi tukamkufuru Mungu hasa pale tunapopatwa na mitihani ya maisha. Ikiwa subira yavuta heri basi kuna kila sababu ya kusubiri na kuvumilia kwakua Mungu wetu yupo kwaajili yetu na atatusaidia kwa majira na wakati wake....

WAIMBAJI WAASWA KUIMBA KWA UPAKO.

Picha
MWIMBAJI/MCH. HAPPY CAMILY Na Mwandishi Wetu , MBEYA . Habari ndugu yangu mpendwa na msomaji wa GOSPEL HEADLINES LEO?  kama ilivyo ada yetu kukuletea habari za injili na wainjilishaji walio ndani na nje ya Tanzania, leo tumekuleta mapokeo ya lile kongamano lililofanyika kule mjini Mbeya katika Kanisa linaloongozwa na Ask/Mch. Adson Mwajunga la TAG Sokomatola Jerusalem Temple siku ya usiku wa tarehe 16 February 2018.     Kwa mujibu wa mashuhuda wetu, lilikua ni kongamano lenye kibali na utukufu wa Mungu. Waimbaji wengi wa muziki huu wa injili wakiongozwa na Mama/Mch. Happy Camily walifika kumwimbia na kumtukuza Mungu pamoja ambapo inaelezwa kuwa miongoni mwa waimbaji hao walioshiriki ni pamoja na: Tumain Mbembela, Iman John, Yakobo Mwamboya, Ikupa Mwambenja, Neema Jackson, The Twins Dadaz, Pinty Melody, Mc Joshua Mwakabela, Emmanuel Mwansasu, Happ Sanga, Ipyana Mwakatika, Afande Bright, Juma Kyando/Kibonge wa Yesu, Patrick Nwaibambe, Ev Mhugo Hantish, Kefa Malima...

MWINJ. MODESTER D HAULE ANATANABAISHA HAYA.

Picha
Na Mwandishi wetu. Njombe . Bwana Yesu apewe sifa watu wa Mungu popote pale mlipo. kama ilivyo ada tunakusogezea habari ya injili na wainjilishaji kutoka ndani na nje ya nchi ya Tanzania. Na leo kutoka nchini Tanzania Mkoani Njombe_Ludewa; GOSPEL HEADLINES LEO inamleta kwenu mwanadada ambaye ni mwimbaji na mwinjilist akiwa na albam yake mpya mkononi iitwayo MUHUME akiwa na maana MTOKE. Akizungumza na mwandishi wetu wa blog ya GOSPEL HEADLINES LEO amesema "ALBAM hii namshukuru sana Mungu kwa kunipa kibali kuikamilisha, bila yeye nisingeweza" Alipoulizwa ni nani mwingine angemshukuru, alijibu "ninao wengi sana wa kuwashukuru lakini nianze kuwashukuru wale wote waliofanikisha kazi hii ya albamu kukamilika, kwanza mtengeneza audio hii Moses Mlowetoka pale Njombe aliweza kunivumilia sana. lakini pia Director Hinju Ze One aliye husika katika kukamilisha DVD hii"      Kazi hii ndugu msomaji unaweza kuipata moja kwa moja kwemye mtandao wa youtube.  Tazama ...

WAIMBAJI MKOANI MBEYA WAPANIA.

Picha
 Na Mwandishi wetu . Mbeya,  kama ilivyo ada ndugu msomaji wa blog yetu pendwa ya GOSPEL HEADLINE LEO, Leo naendelea kukusogezea headline juu ya maandalizi ya waimbaji kwa umoja wao wa Mkoa wa Mbeya na Songwe kuelekea siku ya mkesha wa tar 16 mwezi february 2018 ambapo Umoja huo umeandaa kongamano kubwa la aina yake litakalo fanyika tar tajwa hapo juu kuanzia majira ya saa 2 jioni hadi asubuhi. Kongamano hilo litahusisha waimbaji pamoja na chungaji kadhaa ambao watachukua nafasi za karama zao kumtukuza MUNGU aliye hai.   Kwa taarifa hiyo unaalikwa ewe mkazi wa maeneo ya Mbeya mjini na maeneo ya jirani na mahali popote unapoipata taarifa hii ya kwamba unakaribishwa sana pasipo kiingilio chochote. Picha hizi ni kwa hisani ya HINJU ZE ONE, Film Director  NYOTE MNAKARIBISHWA. ==== TANGAZO JE, UNAHITAJI KUTANGAZA HABARI YAKO HAPA www.hantishmhugo.blogspot.pe ? KAMA NI "NDIO" TUTUMIE EMAIL YAKO KWENDA hantishmhugo@gmail.com AU UJUMBE/PIGA/...

WAIMBAJI WA INJILI ZAIDI YA 200 MKOANI MBEYA NA SONGWE KUKUTANA PAMOJA.

Picha
Na Mwandishi wetu. MBEYA Waimbaji wa nyimbo za injili wanao jumuishwa na umoja wa waimbaji mkoa wa Mbeya na Songwe wapanga kukutana pamoja katika kongamano lao la kusifu na kumwabudu Mungu. Kongamano hilo linapangwa kufanyika mkoani Mbeya, Sokomatola katika kanisa la T.A.G JERUSALEM TEMPLE . ni tar 16 February 2018 kuanzia saa 8:00 pm hadi Asubuhi. Pamoja na ratiba zote hizo, Umoja huo umetenga na muda wa maombi na maombezi. Hivyo nyote mnakaribishwa . kwa wenye shida na magonjwa sugu wataombewa.   miongoni wa waimbaji 200 hao ni pamoja na Tumaini Mbembela, Iman John, Ev Mhugo Hantish, Onesmo Nickodem, Jj Lwiza, Neema Jackson, Ikupa Mwambenja, Yakobo Mwamboya, Asifiwe Ndendya, Afande Bright Mbwilo, na wengine kama picha zinavyooneshwa hapo chini,  NYOTE MNAKARIBISHWA