Mr. Marco Mnanago - Usilie Mama (Official Audio)

Na Mwandishi Wetu.

IRINGA.

Habari yako mpenzi msomaji wetu wa GOSSPEL HEADLINES LEO?

Ni
siku nyingine tena iliyochukua nafasi maishani mwetu ambapo leo
tunamleta kwenu mwimbaji wa nyimbo za injili aitwaye Mr.MARCO MINANAGO
kutoka mkoani Iringa, ambaye leo anautambulisha rasmi wimbo wake hapa
GOSPEL HEADLINES LEO. Wimbo uitwao USILIE MAMA umetengenezwa katika
studio za 2Star Records katika mikono bora ya mtayarishaji Kay B.

   Akizungumza na GOSPEL HEADLINES LEO, Minanago amesema "wimbo
huu wa USILIE MAMA umekua na maana kubwa sana kwangu kwasababu mama ni
jeshi kubwa. Hivyo nimemtumia mama ili kutuwakilisha sote ya kwamba
hatutakiwi kukata tamaa tupatwapo na majaribu."

 Akiongeza zaidi, Mr Marco amesema
"hakuna haja ya kulia hadi tukamkufuru Mungu hasa pale tunapopatwa na
mitihani ya maisha. Ikiwa subira yavuta heri basi kuna kila sababu ya
kusubiri na kuvumilia kwakua Mungu wetu yupo kwaajili yetu na
atatusaidia kwa majira na wakati wake."

   Lakini pia Mr.
Minanago ameongeza kua yupo mbioni kukamilisha na kuachia "Album" mpya
ambayo ndiyo itakayo beba ujumbe huo wa USILIE MAMA. Hivyo
amewasihi wafuasi wa huduma yake ya uimbaji kwamba wakae tayari muda
wowote kuanzia sasa ataachia "Album" hiyo, wajiandae kuipokea.

   Kwa mawasiliano zaidi kuhusu Mr. Marco Minanago unaweza kumpata kwa:

Simu/WhatsApp +255675562922

FaceBook - Minanago Junior

Instagram - @marco_charles

     

 TAZAMA WIMBO HUU HAPA..

 


 

TANGAZO

JE, UNAHITAJI KUTANGAZA HABARI YAKO HAPA www.hantishmhugo.blogspot.pe?

KAMA NI "NDIO" TUTUMIE EMAIL YAKO KWENDA hantishmhugo@gmail.com AU UJUMBE/PIGA/WHATSAPP0768788303.

gospelheadline@2018

"The voice to the voiceless"

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

SOMO:KUSIFU NA KUABUDU KATIKA BIBLIA.

HISTORIA YA MITUME WA YESU KRISTO NA VIFO VIFO

SOMO: MAONO NA NDOTO