WAIMBAJI WAASWA KUIMBA KWA UPAKO.
MWIMBAJI/MCH. HAPPY CAMILY |
MBEYA.
Habari ndugu yangu mpendwa na msomaji wa GOSPEL HEADLINES LEO?
kama ilivyo ada yetu kukuletea habari za injili na wainjilishaji walio ndani na nje ya Tanzania, leo tumekuleta mapokeo ya lile kongamano lililofanyika kule mjini Mbeya katika Kanisa linaloongozwa na Ask/Mch. Adson Mwajunga la TAG Sokomatola Jerusalem Temple
siku ya usiku wa tarehe 16 February 2018.
Kwa mujibu wa mashuhuda wetu, lilikua ni kongamano lenye kibali na utukufu wa Mungu. Waimbaji wengi wa muziki huu wa injili wakiongozwa na Mama/Mch. Happy Camily walifika kumwimbia na kumtukuza Mungu pamoja ambapo inaelezwa kuwa miongoni mwa waimbaji hao walioshiriki ni pamoja na: Tumain Mbembela, Iman John, Yakobo Mwamboya, Ikupa Mwambenja, Neema Jackson, The Twins Dadaz, Pinty Melody, Mc Joshua Mwakabela, Emmanuel Mwansasu, Happ Sanga, Ipyana Mwakatika, Afande Bright, Juma Kyando/Kibonge wa Yesu, Patrick Nwaibambe, Ev Mhugo Hantish, Kefa Malimali na wengine wengi.
PICHA KWA HISANI YA HINJU ZE ONE, DH
Ev Mhugo Hantish akiimba.....
Mr. Christopher Fred30 akiimba.....
...... Roho wa Bwana anaendelea kushuka.....
<.....Katibu Kiongozi wa umoja wa waimbaji wa Mkoa wa Mbeya na Songwe, Tumain Mbembela akitoa mwongozo fulani......>
....wingu linashuka.......
<...Mc. Patrick Mwaibambe akiongoza shughuli...
....mambo ni kama hivi....
Mwimbaji/Mch. Happy Camily akihubiri Neno ....
KUTOKA KUSHOTO: Mc. Neema Jackson, Ev Mhugo Hantish, Katibu Tumain Mbembela na Dir. Hinju Ze One....>
Aidha pamoja na matukio yote hayo, Mch na Askofu wa kanisa hilo alisisitiza katika mahubiri yake huku akitumia baadhi ya vifungu vya Biblia na kusema kuwa waimbaji wa muziki wa injili wanatakiwa kumwomba sana Mungu awajalie kuwa na ROHO MTAKATIFU katika utunzi wa nyimbo zao likini pia aliongezza zaidi na kusema - "waimbaji ni muhimu kumsihi sana Mungu wenu awajalie kuimba nyimbo zenye upako, zinazoponya mioyo, sio zinazoburudisha miili hii ya nje."
lakini pia sehemu ya mahubiri ya Mch. Sephania Mwakajinga yaligusa zaidi kwenye mambo/vitu ambayo/ambavyo mwimbaji katika Roho na kweli anapaswa kuvikwepa, ambavyo ni pamoja na: Epuka kutanguliza fedha kwenye huduma yako, Epuka wanawake au wanaume katika huduma yako na mengine mengi.
Kupitia Blog hii naamini msomaji tumeweza kukufanya mshiriki wa kongamano hilo ambalo liliacha historia kubwa Jijini mbeya. Kwa matukio na habari nyingi ka hizi, usiache kutufuatilia comhttp://hantishmhugo.blogspot.com. Ubarikiwe sana.
TANGAZO
JE, UNAHITAJI KUTANGAZA HABARI YAKO HAPA www.hantishmhugo.blogspot.pe?
KAMA NI "NDIO" TUTUMIE EMAIL YAKO KWENDA hantishmhugo@gmail.com AU UJUMBE/PIGA/WHATSAPP0768788303.
gospelheadline@2018
"The voice to the voiceless"
Maoni
Chapisha Maoni