MWINJ. MODESTER D HAULE ANATANABAISHA HAYA.
Bwana Yesu apewe sifa watu wa Mungu popote pale mlipo. kama ilivyo ada tunakusogezea habari ya injili na wainjilishaji kutoka ndani na nje ya nchi ya Tanzania. Na leo kutoka nchini Tanzania Mkoani Njombe_Ludewa; GOSPEL HEADLINES LEO inamleta kwenu mwanadada ambaye ni mwimbaji na mwinjilist akiwa na albam yake mpya mkononi iitwayo MUHUME akiwa na maana MTOKE. Akizungumza na mwandishi wetu wa blog ya GOSPEL HEADLINES LEO amesema "ALBAM hii namshukuru sana Mungu kwa kunipa kibali kuikamilisha, bila yeye nisingeweza" Alipoulizwa ni nani mwingine angemshukuru, alijibu "ninao wengi sana wa kuwashukuru lakini nianze kuwashukuru wale wote waliofanikisha kazi hii ya albamu kukamilika, kwanza mtengeneza audio hii Moses Mlowetoka pale Njombe aliweza kunivumilia sana. lakini pia Director Hinju Ze One aliye husika katika kukamilisha DVD hii"
Kazi hii ndugu msomaji unaweza kuipata moja kwa moja kwemye mtandao wa youtube.
Tazama hapa wimbo huu uitwao MWANADAMU WA KWANZA.http://hantishmhugo.blogspot.com
====
TANGAZO
JE, UNAHITAJI KUTANGAZA HABARI YAKO HAPA www.hantishmhugo.blogspot.pe?
KAMA NI "NDIO" TUTUMIE EMAIL YAKO KWENDA hantishmhugo@gmail.com AU UJUMBE/PIGA/WHATSAPP0768788303.
gospelheadline@2018
"The voice to the voiceless"
Maoni
Chapisha Maoni