HABARI: WIMBO WA ''IGUSE TANZANIA'' WA Ev Mhugo Hantish WATAMBULISHWA RASMI LEO.
NA MWANDISHI WETU,
Haleluya mtu wa Mungu popote pale ulipo 🌍 unayetufuatilia kupitia nyanja zetu za mitandao mbalimbali ya kijamii.
Kwa mara ya kwanza mbele yako leo tunautambulisha wimbo huu wa IGUSE
TANZANIA ikiwa ni ujumbe unaashiria ya kwamba tunamhitaji Mungu juu ya
mustakabali wa maisha yetu na Taifa kwa ujumla. Wimbo huu umeimbwa na Ev
Mhugo Hantish.
Hivyo tunakusihi tuweke tofauti za makabila, Dhehebu, Dini au Rangi na kisha tushikamane sote kumwomba Mungu AIGUSE NCHI YETU YA TANZANIA hasa katika maeneo yenye viashiria vya uvunjifu wa amani.
Kwa hisani ya DH- DIRECTOR HINJU.
"Namshukuru Mungu kwa neema yake aliyoiachilia juu ya Maisha yangu hasa
kwa kuniamini na kunipa kusudi la kutumika kwa njia ya uimbaji. Leo
mbele yako nimeutambulisha wimbo wetu uitwao IGUSE TANZANIA. Natamani
kila mtazamaji na msikilizaji wote kwa Umoja tujinyenyekeze mbele za
Mungu na kumwomba AIGUSE NCHI YETU YA TANZANIA. Hakuna Asiye fahamu ya
kwamba kwa sasa nchi yetu inapita katika Kipindi kigumu sana. Maisha ya
kila mmoja mmoja yapo hatarini sana huko mbeleni ikiwa waombaji,
waimbaji na wahubiri hatutagusia suala hili Zito la kuiombea nchi yetu
pamoja na viongozi wa nchi na wananchi kwa ujumla. Ni wakati sasa wa
Kuweka tofauti zetu za kidini, Dhehebu, Kabila na rangi na kisha
kusimama pamoja katika jambo hili la mauaji, utekaji, upotevu wa
rasilimali watu, pamoja na viashiria vyote vya uvunjifu wa amani.
Ee Mungu IGUSE TANZANIA." - Ev Mhugo Hantish
Wimbo huu umesapotiwa na www.hantishmhugo.blogspot.com na Director HINJU
ZE ONE.
Tupate kupitia:
Instagram: Gospel Headlines Leo
Facebook: Gospel Headlines Leo
Tuandikie email kwa hantishmhugo@gmail.com au gheadlinesleo@gmail.com
Au kwa mawasiliano +255768788303
Ubarikiwe sana..

Maoni
Chapisha Maoni