MWAMINI MUYERO - YESU USIFIWE
Na Mwandishi Wetu,
Dar-Es-Salaam,
Baada ya siku chache zilizopita kuachia wimbo wake mpya uitwao Yesu
Usifiwe mwimbaji wa nyimbo za Injili Mwamini Muyero sasa ameachia video
ya wimbo huo ikiwa imeongozwa na director Mbangwa Hassan, ukiwa ni wimbo
maalum wa sifa kwa ajili ya Pasaka, Muziki huu umetayaarishwa ndani ya
studio za Soft Records chini ya mikono ya prodyuza Pitshou Mesha.
“Yesu Usifiwe ni wimbo wa Sifa nikiwakumbusha watu, hasa wale
wanaopitia katika shida na mambo magumu, wimbo huu ukawe nuru na nguzo
ya matumaini katika maisha yao na nawasihi watambue kuwa hakuna
lisilowezekana kwa Yesu maana yote aliyamaliza pale msalabani, waendelee
kumtumainia Mungu naye atatenda miujiza kwa zaidi ya wanavyofikiria,
Ameen.” – Mwamini Muyero
Ikumbukwe kuwa mwimbaji Mwamini Muyero tayari ana albamu iitwayo
Nimepata Pumziko aliyoachia mwaka 2016 ikiwa kwenye mfumo wa Audio
CD na DvD ikiwa inasambazwa na yeye mwenyewe na kupatikana kwenye maduka
ya wasambazaji kote nchini.
Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu hapa nikiamini kuwa utabarikiwa zaidi, Ameen.
Download Audio
Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Mwamini Muyero kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 769 698 909
Facebook: Mwamini Muyero
Instagram: @officialmwamini
YouTube: Mwamini Muyero
credit to www.gospomedia.com
Maoni
Chapisha Maoni